Mwisho wa mwaka unakaribia na kila ifikapo tarehe kama hizi wengi wetu huanza kujitathimini nini tulichoweza kufanya kwa mwaka mzima, hapa Tanzania Tech pia tunakuleta countdown za mambo mbalimbali yahusuyo teknolojia ambayo kwa namna moja ama nyingine yameweza kushika chat kwa mwaka mzima huu wa 2018.
Baada ya kuhesabu channel 10 za YouTube ambazo ni maarufu zaidi kwa hapa Tanzania, sasa ni wakati wa kuzihesabu tovuti 10 zilizo tembelewa zaidi kwa mwaka 2018. Kumbuka list hii inatokana na idadi ya watu waliotembelea tovuti hii kwa mwaka mzima hadi siku ya leo tarehe 7/12/2018, vilevile ni vizuri kufahamu kuwa hapa Tuna angazia tovuti za Tanzania pekee hivyo usishange usipo ona tovuti kama Instagram na Facebook na nyingine kama hizo, basi bila kupoteza muda let’s get to it…
10. ZoomTanzania
Namba 10 kwenye list – Namba 27 Kwa Tanzania Nzima
- Imetembelewa na Watanzania kwa asilimia 85.9%
- United States 1.0%
- Netherlands 0.6%
Tovuti ya ZoomTanzania imeshuka sana chati ukilinganisha na mwaka jana kwani tovuti hiyo ilikuwa namba tatu mwaka 2017 na sasa imeshuka kwa nafasi 7 mfululizo. Pengine ni wakati sasa kampuni ya ZoomTanzania kuangalia tatizo liko wapi kwani kama ni biashara basi inapoteza wateja.
9. Millard Ayo
Namba 9 Kwenye List – Namba 23 Kwa Tanzania Nzima
- Imetembelewa na Watanzania kwa asilimia 83.3%
- China 5.7%
- United States 1.5%
Millard ayo ilikuwa ni tovuti namba moja ya habari hapa Tanzania, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda inaonekana Millard akipambana na YouTube zaidi kuliko tovuti yake kwani kwenye list ya Channel maarufu zaidi Millard ayo ni channel iliyo shikilia nafasi ya pili. Pengine ushauri wangu ni kuwa aendelee kupambana na tovuti yake kwani huwezi jua YouTube inaweza kusitishwa hata kesho, ni vyema kutegemea chako kuliko cha mtu.
8. DJ Mwanga
Namba 9 Kwenye List – Namba 22 Kwa Tanzania Nzima
- Imetembelewa na Watanzania kwa asilimia 96.2%
- Kenya 1.1%
Mwaka jana 2017 tovuti ya DJ Mwanga haikuwepo kwenye chati hii lakini hivi leo tovuti hii imeshikilia namba 8 kwenye list hii pamoja na namba 22 kwa Tanzania nzima. Hongera kwa DJ mwanga na pengine ni wakati sasa wa kuongeza juhudi za dhati kuhakikisha kuwa unafanikiwa zaidi.
7. Tra.go.tz
Namba 7 kwenye List – Namba 19 kwa Tanzania Nzima
- Imetambelewa na Watanzania kwa asilimia 94.3%
- Haijatembelewa na Nchi nyingine yoyote
Ni wazi kuwa watu wengi sasa wamekuwa walipa kodi waaminifu kwani tovuti hii haikwepo kwenye list hii lakini hivi leo imeshikilia namba 7 na Namba 19 kati ya tovuti zinazo tembelewa zaidi Tanzania nzima.
6. Mkekabet
Namba 6 kwenye List – Namba 18 kwa Tanzania Nzima
- Imetambelewa na Watanzania kwa asilimia 99.8%
- Haijatembelewa na Nchi nyingine yoyote
Ukweli ni kwamba kasi ya ujio wa michezo ya kubahatisha imekuwa kubwa sana siku hizi, watu wamekuwa wakiamini bahati zao kuliko hata utendaji wa kazi lakini anyway najua pia hii inasababishwa na matangazo mengi ambayo mkekabet inafanya.
5. Meridianbet
Namba 5 Kwenye List – Namba 16 Tanzania Nzima
- Imetembelewa na Watanzania kwa asilimia 99.9%
- Haijatembelewa na Nchi nyingine yoyote
Kama unavyozidi kuona mapenzi ya Watanzania kwenye michezo ya ku-bet, ni wazi kuwa kama una wazo lolote la biashara ya michezo ya kubahatisha sasa ndio wakati mzuri wa kufanyia kazi wazo lako.
4. M-Bet
Namba 4 Kwenye List – Namba 15 Tanzania Nzima
- Imetambelewa na Watanzania kwa asilimia 96.0%
- United Kingdom 2.7%
- India 0.5%
Hapa sina haja ya kusema mengi sana cha muhimu wewe kujua ni kuwa M-Bet wanaendelea kushikilia namba 4 kama ilivyo kuwa hapa mwaka jana 2017.
3. Ajira.go.tz
Namba 3 Kwenye List – Namba 10 Tanzania Nzima
- Imetembelewa na Watanzania kwa asilimia 92.7%
- China 5.0%
Tovuti hii ya ajira za serikali imeshuka nafasi mbili kwani mwaka jana 2017 tovuti hii ilikuwa ni tovuti namba mbili kwenye list. Lakini pamoja na hayo bado inaendelea kuongoza hapa Tanzania kwani hii ni tovuti ya 10 kutembelewa zaidi kwa Tanzania nzima.
2. Ghafla
Namba 2 Kwenye List – Namba 6 Tanzania Nzima
- Imetembelewa na Watanzania kwa asilimia 22.3%
- Nigeria 26.6%
- Kenya 15.7%
- Uganda 11.6%
- Ghana 9.5%
Kama ulikuwa hujui tovuti ya ghafla hii ni tovuti kama millard ayo, tovuti hii inaleta habari mbalimbali za udaku za Tanzania, kenya na nchi nyingine. Tovuti hii haikwepo kwenye list hii ila kama unavyoweza kuona sasa imeshikilia namba mbili kwenye list hii na Namba 6 kwa Tanzania nzima.
1. JamiiForums
Namba 1 Kwenye List – Namba 5 kwa Tanzania Nzima
- Imetembelewa na Watanzania kwa asilimia 72.4%
- Kenya 5.9%
- United States 4.9%
- South Africa 1.5%
- United Kingdom 1.3%
Tovuti iliyo tembelewa zaidi kwa hapa Tanzania kama ilivyokuwa mwaka jana 2017 ni tovuti ya jamii forums, ongera za dhati kwa wamiliki wa tovuti hii.
Na hizo ndio tovuti 10 zilizotembelewa zaidi hapa Tanzania, kama unataka kujua list ya mwaka jana unaweza kubofya hapa kuweza kujua zaidi Tovuti zilizo tembelewa zaidi kwa mwaka 2017 na pia mwaka 2016.