Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tovuti Inayo Tengeneza Hadi Dollar $300 Kwa Mwezi

Kupitia tovuti hii utaweza kutengeneza hata zaidi ya $300 ukiwa na bidii
Tovuti Inayo Tengeneza Hadi Dollar $300 Kwa Mwezi Tovuti Inayo Tengeneza Hadi Dollar $300 Kwa Mwezi

Habari karibu kwenye makala nyingine ya jinsi ya kutengeneza pesa mtandaoni, kupitia makala hii nitakuonyesha jinsi nilivyoweza kutengeneza tovuti moja ambayo imenisaidia kutengeneza pesa mtandaoni hadi kufikia kiasi cha dollar $300 kwa mwezi.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa Tanzania tech, basi hii itakuwa sio mara yako ya kwanza kusikia kuhusu njia hizi. Pia ningependa ufahamu kuwa njia hii sio njia mpya bali ni njia ambayo tayari nimesha elezea kipindi cha nyuma na hapa nakupa update ya tovuti hiyo kwa sasa.

Advertisement

Kama ulifuatilia makala hii ya tovuti inayo tengeneza dollar 100 kwa mwezi basi lazima utakuwa unajua kuwa tovuti hii inao uwezo wa kutengeneza pesa mtandaoni bila ya kuandika makala yoyote ile. Lakini mbali ya yote tovuti hii inaweza kutengeneza pesa kupitia Google Adsense.

Kama unavyoweza kuona mwezi wa nane, tovuti hii ilikuwa na uwezo wa kutengeneza hadi dollar $100 kwa mwezi. Hii ikiwa ni muda wa miezi minne tokea nilipo tengeneza tovuti hiyo mwezi wa tano.

Update leo Tarehe 12/12/2020

Baada ya miezi mingine minne tokea nilipo onyesha video hiyo hapo juu, leo nakuletea udate ya tovuti hii ambayo nilipata njia nyingine ya kuweza kuongeza kipato kupitia tovuti hiyo. Hadi leo siku ya jumamosi, tovuti hiyo imeweza kutengeneza hadi dollar $300 kwa mwezi.

Kama unavyoweza kuona guys! njia hii inafanyakazi kwa ukakika na inaweza kusaidia kuongeza au kutengeneza kipato mtandaoni. Lakini kabla ya hayo ni muhimu kujua mambo ya msingi sana.

Mambo ya Muhimu Kabla ya Kuanza

Kama nilivyo kwambia, ni muhimu kujua mambo ya msingi ambayo yanaweza kukupa muongozo sahihi ambao utakusaidia kwa baadae. Mambo hayo ni kama yafuatayo

  • Kwa kuanza ni vyema kujua kuwa njia hii inaweza kusaidia kutengeneza pesa mtandaoni lakini inategemea na jinsi utakavyo pata traffic kwenda kwenye blog yako.
  • Kitu kingine ni muhimu sana sana kuwa na subira kwa maana njia hii lazima inafanyakazi tofauti kwa kila mtu, haiwezekani kufanana kwa kila mtu. Mimi naweza kuchukua miezi minne kufanikiwa, lakini wewe ukachukua miezi miwili, Haiwezekani tufanane kwa asilimia 100.
  • Hakuna kitu kirahisi duniani – kama wewe ni mmoja wa watu wanaotafuta njia za kutengeneza pesa mtandaoni kwa haraka basi haupo mahali sahihi, hapa Tanzania tech njia zote zilizopo hapa hutumia muda kufanikiwa na sio vinginevyo.
  • Ni muhimu kuwa na ujuzi angalau kidogo kuhusu maswala ya mtandaoni au kuhusu tovuti kwa ujumla. Bila hivyo utachelewa kufanikiwa japo kuwa utafanikiwa.
  • Ni muhimu kuwa na fikira za kufanikiwa kipesa lakini sio kila mara. Hapa nina maana kuwa ukiwa mtu wa kuwaza pesa kila mara utashindwa kufanya mambo ya muhimu ambayo yanahitaji muda wako zaidi kuliko pesa.
  • Wekeza muda wako kuhakikisha unafanikiwa. Kwenye hili ni muhimu sidhani kama nahitaji kukwambia tena kwani point zote hapo juu zinalenga kwenye hili, siku zote fikiria kuwekeza kwenye kujifunza na kuelewa jinsi kitu kinavyofanya kazi.
  • Na mambo mengine unaweza kusoma hapa.

Jinsi ya Kupata Tovuti Hii

Tovuti Inayo Tengeneza Hadi Dollar $300 Kwa Mwezi

Kama unataka kujua zaidi kuhusu tovuti hii nakushauri usome makala iliyopita hapa. Baadhi ya sifa nyingine za tovuti hii ni pamoja na.

  • Mfumo huu unaweza kutafuta makala za aina yoyote na kuziweka kwenye website hii bila wewe kuandika makala ya aina yoyote.
  • Unaweza kufanya mfumo huu uchukue makala kutoka website yoyote ile na unaweza kuweka website nyingi kadri uwezavyo.
  • Mfumo huu unakubaliwa matangazo na Google Adsense (Ni muhimu kusubri siku kwa muda kabla ya kuoba matangazo kwa mara ya kwanza), pia unakuja na sehemu za matangazo ambazo zinafanya utengeneze pesa kwa haraka,
  • Utaweza kuchukua content kwa kubofya link moja tu kila saa unapotaka kuchukua content hizo, yaani utaweza kupublish content kwa kubofya link.
  • Mfumo huu unakuja na Size ya MB 2 hivyo unaweza kuhost kwenye hosting yoyote.
  • Unaweza kutengeneza website kama Google ambayo ni search engine na unapo search website nyingine zinaonekana kama matokeo.
  • Huna haja ya kuwa na kompyuta kutumia mfumo huu kwani unaweza kuendesha kwa kutumia simu yako ya mkononi.
  • Na mengine mengi..

Unaweza Kuangalia Mfumo Huo Hapa

NB: Tovuti hii tunategemea kuiamisha siku za karibuni na tunatengeneza tovuti kama hii bora zaidi kwaajili ya kazi.

Unaweza kupata mfumo huu kwa bei rahisi ya 135,000 ikiwa pamoja na domain yoyote ya .COM pamoja na hosting ya GB 100 kwa mwaka mzima. Pia utasaidiwa kuanya setup ya mfumo huu ikiwa pamoja na kuchagua aina ya makala ambazo zitakuwa bora kwako.

Unaweza kupata mfumo huu kwa kuwasiliana kupitia ukurasa hapa, au unaweza kutuma meseji ya WhatsApp kupitia namba hapa. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu ya biashara hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use