Kampuni ya Toshiba ni moja kati ya kampuni zilizokuwa zinatengeneza laptop nzuri sana kwa kipindi hicho. Lakini baada ya miaka 35 ya kutengeneza laptop hatimaye kampuni hiyo imeondoka rasmi kwenye biashara ya kutengeneza laptop.
Inasemekana kuwa kampuni ya Toshiba ilitoka kimya kimya kwenye biashara hiyo wiki iliyopita, ikiwa ina kamalisha harakati za miaka 35 kwa kuhamisha hisa zake zilizobaki kwenye biashara yake ya PC kwenda kwa kampuni ya Sharp.
Hata hivyo inasemekana kuwa, Miaka miwili iliyopita, Toshiba aliuza asilimia 80.1 ya biashara yake ya PC kwa kampuni ya Sharp, kwa dola za marekani milioni 36, hata hivyo Sharp ilibadilisha jina la idara hiyo kwenda kwenye jina la Dynabook.
Hivi karibuni Kampuni ya Sharp imekamilisha ununuzi wa asilimia 19.1 ya hisa za Toshiba zilizobaki hapo Juni 2020, na kufanya kampuni ya Toshiba kutokuwa na hisa zozote kwenye kampuni ya Dynabook.
Kukamilika kwa mpango huo wa mauziano kunafanya Dynabook ambayo ilikuwa ni muunganiko wa Toshiba na kampuni ya Sharp, kumilikiwa kwa asilimia 100 na kampuni ya Sharp na kufanya Toshiba kuondoka rasmi kwenye biashara hii ya utengenezaji wa laptop.
Ni wazi kuanzia sasa hutoweza kuona tena Laptop mpya yenye jina la Toshiba na badala yake utaendelea kuona laptop za Dynabook ambazo zinatengenezwa na kampuni ya Sharp.