Baada ya majaribio ya muda mrefu kampuni ya Apple hapo jana imeanza kutoa toleo jipya la iOS 10.3 kwenda kwa watumiaji wa vifaa mbalimbali vya Apple. Toleo hilo jipya linakuja na maboresho kadhaa yatakayo ongeza ufanisi mzuri wa simu yako.
Moja ya Maboresho makubwa ni pamoja na uwezo wa kutafuta (Air pods) wireless headphone za apple kwa kutumia GPS au kwa kutoa mlio maalum, hii ni muhimu pale unapo poteza headphone hizo kwani wote tunajua jinsi gani earphone hizo zilivyokuwa ndogo. Vilevile maboresho mengine ni kwenye programu ya SIRI ambapo sasa utaweza kupata matokeo mbalimbali ya michezo, kulipa bili mbalimbali pamoja na kuita usafiri wa Uber. Kingine ni kwa upande wa Apple Music, sasa utapata uwezo wa kuona baadhi ya playlist mpya pamoja na shortcuts ambazo zinaonyesha programu uliyo tumia mara ya mwisho vile vile sasa utaweza kuona taarifa za nyimbo unayosikiliza kwenye sehemu ya Now Playing screen.
Kumbuka kabla ya kufanya update ni vyema kuweka data zako sehemu nyingine (fanya backup) kwani unaweza ukapoteza baadhi ya vitu. Ili kuangalia kama kifaa chako kina update hizo ingia kwenye Settings kisha bofya ‘Software Update’ utapata update hizo, lakini kama pia kwa namna moja ama nyingine umeshindwa ku-update unaweza kudownload update hizo kwa kutumia link hapo chini. (Kumbuka kutumia link yenye jina la kifaa chako)
- 9.7-inch iPad 2017 (WiFi)
- 9.7-inch iPad 2017 (Cellular)
- 12.9-inch iPad Pro (WiFi)
- 12.9-inch iPad Pro (Cellular)
- 9.7-inch iPad Pro (WiFi)
- 9.7-inch iPad Pro (Cellular)
- iPad Air 2 (6th generation WiFi)
- iPad Air 2 (6th generation Cellular)
- iPad Air (5th generation WiFi + Cellular)
- iPad Air (5th generation WiFi)
- iPad Air (5th generation CDMA)
- iPad (4th generation CDMA)
- iPad (4th generation GSM)
- iPad (4th generation WiFi)
- iPad mini 2 (WiFi + Cellular)
- iPad mini 2 (WiFi)
- iPad mini 2 (CDMA)
- iPad mini 3 (China)
- iPad mini 3 (WiFi)
- iPad mini 3 (Cellular)
- iPad mini 4 (WiFi)
- iPad mini 4 (Cellular)
- iPhone 5 (CDMA)
- iPhone 5 (GSM)
- iPhone 5c (CDMA)
- iPhone 5c (GSM)
- iPhone 5s (CDMA)
- iPhone 5s (GSM)
- iPhone 6
- iPhone 6 Plus
- iPhone 6s
- iPhone 6s Plus
- iPhone 7 (iPhone9,1)
- iPhone 7 Plus (iPhone9,2)
- iPhone 7 (iPhone9,3)
- iPhone 7 Plus (iPhone9,4)
- iPhone SE
- iPod touch (6th-generation)
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.