Microsoft ipo mbioni kutoa toleo jipya la Windows 10, toleo ambalo linasemekana kuja na maboresho kadhaa ikiwa pamoja na mpangilio mpya wa kuzuia kiasi cha GB 7 kwenye kompyuta yako. Kwa mujibu wa mtandao wa Techradar, mpangilio huo mpya utakuwa unahitaji kompyuta zinazopokea mfumo huo mpya kuwa na zaidi ya GB 7 ili kuweza kupokea mfumo huo.
Kwa mujibu wa mtandao huo, inasemekana kuwa GB hizo 7 zitakuwa ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa masasisho mapya ya Windows 10 yanaweza kupakiwa bila kuwa na tatizo la nafasi kwenye kompyuta yako. Inasemekana nafasi hiyo hautoweza kuweka kitu chochote na itakuwa ni kwa ajili ya matoleo hayo mapya ya Windows 10.
Bado haijajulikana kama kompyuta ambazo hazina nafasi hiyo ya GB 7 kama zitakuwa na uwezo wa kupata sasisho hilo jipya la Windows 10 ambalo linategemewa kuja miezi ya karibu.
Mbali na hayo maboresho mengine ambayo yanategemewa kwenye mfumo huo mpya wa Windows 10 version 1903, ni pamoja na uwezo mpya wa kusimamisha masasisho (Updates) mapya kwa muda wa wiki moja, Hii itasaidia sana hasa kwa wale ambao kompyuta zao zina tafuta masasisho mapya pale tu kompyuta inapounganishwa na Internet.
Kwa sasa kama unataka kujua baadhi ya mabadiliko yanayokuja kwenye toleo hilo jipya la Windows 10 version 1903 unaweza kuangalia video hapo chini.
Kama unataka kuinstall mfumo huu kwa sasa ili uweze kujaribu baadhi ya sehemu hizi kwenye kompyuta yako, unaweza kufuata hatua HAPA, kisha utaweza kuona update kwenye kompyuta yako na utakuwa tayari kujaribu matoleo mpya ya Windows 10 kabla hajatoka rasmi.
naomba kujua ubora wa kutumia window 10