Programu ya VLC imekua ni programu tegemezi sana kwenye vifaa mbambali kama kompyuta pamoja na simu za mkononi, pengine hii ni kutokana na ubora wa programu hiyo ambayo sasa imezidi kuwa bora zaidi.
Hivi karibuni unaweza kujikuta unategemea zaidi programu ya VLC kuliko programu nyingine kwenye kifaa chako na hii ni kwa sababu VLC sasa imezidi kuwa bora zaidi pamoja na kuongezewa uwezo zaidi kwenye toleo jipya la VLC 3.0
Toleo hilo jipya limeongezewa mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na uwezo wa kucheza video zenye uwezo wa 8K, uwezo wa kusoma video za HDR, uwezo wa sauti kupitia HMDI Audio, uwezo wa kuonyesha video za nyuzi 360, uwezo wa kuonyesha DVD za mfumo wa HD pamoja na uwezo wa sauti wa 3D audio.
Toleo hilo jipya la VLC 3.0 tayari linapatikana kupitia tovuti ya VideoLAN kwa wanaotumia Kompyuta na kama unatumia programu hii kwenye simu yako basi unaweza kudownload kupitia soko husika kati ya Play Store au App Store.
- VLC – Kompyuta
- VLC – Android
- VLC – iOS