Mwaka jana kampuni ya LG ilizindua simu yake mpya ya LG V30 ambayo ilikuwa simu bora sana hasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kamera. Sasa Kampuni ya LG imerudi tena kupitia mkutano wa MWC 2018 ambapo sasa inakuja na toleo jipya la simu hiyo ya LG V30S.
Simu hii haina tofauti sana na simu ya LG V30, bali simu hii imeongezewa mambo mbalimbali kama vile mfumo wa AI au artificial intelligence ikiwa ni pamoja na muonekano mpya na watofauti kidogo.
Simu hii inakuja na kioo kikubwa cha inch 6 pamoja na processor ya Qualcomm Snapdragon 835 huku kwa nyuma ikiwa na kamera mbili za nyuma moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 13 yenye uwezo wa kuchukua picha za wide-angle. Kwa mbele LG V30S inakuja na kamera ya Megapixel 5.
Kuna tofauti ndogo sana kwenye simu hii ya LG V30S ThinQ na LG V30 ya mwaka jana na kwa mujibu wa wataalam utofauti ulipo kwenye simu hizi ni sehemu iliyo ongezwa kwenye LG V30S ni sehemu ya AI au Artificial Intelligence ambayo kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu.