Hivi karibuni kuligundulika aina mpya ya virusi ambavyo vilikuwa na uwezo wa kuzuia programu mbalimbali za simu yako ya iphone kufanya kazi. Virusi hivyo vilivyokuwa vinatokana na neno la kihindi vinauwezo wa kuzima programu za ujumbe kama vile programu za iMassage, WhatsApp, Pamoja na FB Messenger.
Sasa hivi leo kampuni ya Apple imetoa toleo jipya la mfumo wa uendeshaji wa iOS 11.2.6 toleo ambalo litakuwa na uwezo wa kuondoa tatizo hilo pamoja na virusi hivyo. Hata hivyo Apple pia imetoa toleo jipya la mifumo ya vifaa vyake vingine kama watchOS, tvOS, pamoja na macOS.
Unaweza kuangalia update za kifaa chako sasa ili kuweza kulinda vifaa vyako vya Apple dhidi ya virusi hivyo vinavyotokana na neno la lugha ya kihindi (Telugu) . Kama unataka kuangalia update hizo, bofya sehemu ya Settings > alafu General > Software Update kisha download na install update hizo kwenye simu yako au vifaa vyenye kutumia mfumo wa watchOS, tvOS, pamoja na macOS.