Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia smartphone au umekuwa msomaji wa Tanzania Tech basi lazima umesha sikia tukisema sana kuhusu processor za Mediatek na Snapdragon. Sasa kutokana na mijadala mbalimbali mitandaoni kuhusu processor hizi mbili leo nimeona nikuletee makala fupi yenye kuonyesha tofauti kati ya processor za Mediatek na Snapdragon.
Kupitia makala hii sitoingia ndani sana na kuanza kuzungumza historia ya kampuni hizi mbili bali nitatumia muda huu kukwambia vitu vya muhimu ambavyo nadhani vinaweza kufanya uweze kuona tofauti kati ya processor hizo mbili. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie tofauti hizi.
Utengenezaji
Kwa kuanza labda tuongelee tofauti ya utengenezaji wa processor za Mediatek Helio na Qualcomm Snapdragon. Kwa upande huu kampuni zote mbili hazitengenezi processor zake zenyewe bali kampuni hizi mbili zote hufanya ubunifu wa mitindo ya processor ikiwa pamoja na kufanya tafiti mbalimbali na baadae processor hizo hutengenezwa na kampuni inayoitwa ARM Holdings.
Tofauti kubwa kwenye upande wa utengenezaji wa Processor hizi ni upande wa GPU, Mediatek hutumia GPU za Mali ambazo hizi pia utengenezwa na ARM Holdings, lakini kwa upande wa Snapdragon wao hutumia GPU za Adreno ambazo hizi hutengenezwa na Qualcomm wenyewe.
Hivyo basi, utaweza kuona tofauti ya utengenezaji wa processor za Mediatek Helio na Qualcomm Snapdragon ni kuwa GPU za Snapdragon hutengenezwa na Qualcomm wenyewe wakati GPU za Mediatek hutengenezwa na ARM na ndio maana mara nyingi GPU hizi huitwa ARM Mali (GPU).
Uwezo wa GPU
Kutokana na Qualcomm kutengeneza GPU zake yenyewe mara nyingi GPU za Qualcomm ambazo ni Adreno huwa na uwezo mzuri zaidi tofauti na GPU za Mali ambazo hutumiwa kwenye processor za Mediatek. Hii inaweza kuonekana kwenye baadhi ya simu hasa kwa wale wapenzi wa Game wanaweza wakawa wanajua zaidi kuhusu hili, mara nyingi simu zenye GPU za Mali huwa na matatizo ya kupata moto sana tofauti na GPU za Adreno hasa unapokuwa unacheza game zenye uwezo mkubwa.
Lakini pamoja na hayo GPU za Mali huwa na uwezo mkubwa wa speed tofauti na GPU za Adreno ndio maana mara nyingi simu zenye GPU za Mali hupata joto kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha chaji kuendesha GPU yenyewe unapokuwa unacheza game, ukilinganisha na GPU za Adreno kutoka Qualcomm Snapdragon ambazo hutumia kiasi kidogo cha chaji kuendesha GPU zake.
Uwezo wa CPU
Kwa upande wa uwezo wa CPU mpaka sasa najua unajua kuwa kampuni zote hzitengenezi processor zake zenyewe isipokuwa GPU za Adreno zenyewe hutengenezwa na kampuni ya Qualcomm yenyewe.
Lakini pamoja na hayo kampuni ya Qualcomm yenyewe baada ya kupokea processor zake kutoka kwa kampuni ya ARM Holdings hufanyia mabadilIko na maboresho ya CPU na kuziongezea uwezo zaidi na kutengeneza processor zake zenye ubora zaidi kama vile Kryo CPU ambazo hizi ni sawa na kusema ni CPU zilezile lakini zimeongezewa uwezo zaidi na kampuni ya Qualcomm.
Kwa upande wa Mediatek yenyewe huchukua processor hizo na kuzitumia kama zilivyo hivyo utaweza kuona kuwa processor za Qualcomm Snapdragon zinaweza kufanya kazi vizuri zaidi kwenye upande wa CPU, tofauti na processor za Mediatek ambazo hutumika kama zilivyo kutoka kampuni ya ARM Holdings.
Gharama
Sasa kutokana na kampuni ya Qualcomm kubadilisha kidogo processor zake hii upelekea processor za Qualcomm Snapdragon kuwa za gharama zaidi kuliko zile za Mediatek na unaweza kuona hili kwenye simu nyingi zenye processor za Qualcomm Snapdragon.
Mara nyingi simu zenye processor hizo huwa zinapatikana kwa bei ghali zaidi kuliko simu zenye processor za Mediatek, hii inatokana na gharama za zaidi ambazo kampuni ya Qualcomm huingia kutengeneza processor hizo za Snapdragon hasa kwenye upande wa CPU.
Utumiaji
Sasa baada ya kuongelea hayo hebu tuongelee kidogo kuhusu utumiaji, Mara nyingi simu zenye processor za Mediatek huchelewa sana kupata matoleo mapya ya mifumo ya uendeshaji tofauti na simu zenye processor za Snapdragon.
Hii hutokana na mfumo mzima unaotumiwa na Mediatek sio mifumo huru (Open Source) hivyo ni ngumu kwa wabunifu wa programu kuweza kupata nafasi ya kutengeneza kwa haraka mifumo ya uendeshaji kwaajili ya simu zenye processor hizo. Lakini kwa upande wa Snapdragon hakuna matatizo yoyote ya simu zenye processor hizo kuchelewa kupata matoleo mapya ya mfumo wa uendeshaji.
Battery
Pia vile vile kwa sababu nilizo kwambia hapo awali, Mara nyingi simu zenye processor za Mediatek hutumia chaji zaidi ya simu zenye processor za Qualcomm Snapdragon hii hutokana na kuwa processor hizi hutumia Core nyingi zaidi kwenye chipset zake hivyo hutumia chaji zaidi kuweza kuendesha processor hizo.
Pia kwa upande wa GPU kama nilivyo kwambia awali simu zenye processor za Mediatek hutumia GPU zenye Speed zaidi hivyo speed kubwa ni lazima iende sawa sawa na uwezo wa battery. “More speed more battery”.
Hitimisho
Kama unavyoweza kuona kwa namna moja ama nyingine processor za Snapdragon ni bora kuliko processor za Mediatek, lakini sio kwamba processor za Mediatek ni mbaya, HAPANA. Processor zote mbili zinaweza kufofautiana uwezo kwenye kila aina ya simu hivyo kuna simu nyingine unaweza ukakuta inayo processor ya Snapdragon lakini ikapitwa kila kitu na simu yenye processor ya Mediatek.
Pia kwenye upande wa GPU, sio kila simu yenye processor ya Qualcomm Snapdragon basi moja kwa moja inakuwa inatumia GPU ya Adreno bali zipo simu nyingi zenye kutumia processor hiyo na zinatumia GPU ya ARM Mali, Samsung ni moja ya mfano wa simu zinazokuja na GPU ya Mali kutokana na processor zake za Exynos ambazo pia hutumia GPU za ARM Mali.
Thats it.. Guys hiyo ndio tofauti kati ya processor za Mediatek Helio na Qualcomm Snapdragon, kama kuna mahali popote hujaelewa unaweza kuuliza kupitia sehemu ya moani hapo chini, Mpaka next time endelea kutembelea Tanzania Tech kwa habari zaidi za teknolojia. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua kuhusu mambo yote ya muhimu kuhusu Jumia Tanzania.