Tofauti ya Battery za Simu Zenye Teknolojia ya Li-ion na Li-Po

Zifahamu faida na hasara za battery za Li-ion na Li-Po kwenye smartphone yako
Tofauti ya Battery za Simu Zenye Teknolojia ya Li-ion na Li-Po Tofauti ya Battery za Simu Zenye Teknolojia ya Li-ion na Li-Po

Ni mara nyingi sana tukiangalia sifa mbalimbali za simu utakuta tunasoma kuwa uwezo wa battery ni Li-ion 6000 mAh au labda Li-Po 6000 mAh. Lakini je unajua maana ya Li-ion au Li-po..? na Je unajua tofauti ya battery hizi kwenye simu yako.?

Kujibu maswali hayo leo nimekuandalia makala hii ya je wajua ambayo natumaini mpaka mwisho utaweza kujua tofauti ya battery hizi ikiwa pamoja na sifa zake. Lakini kabla ya kusoma makala hii unaweza kusoma makala yetu iliyopita ya mambo matano ambayo yanafanya battery ya simu yako kuharibika kwa haraka.

Advertisement

Kama tayari umesha soma makala hiyo basi moja kwa moja twende kwenye makala hii ambayo nitakuonyesha tofauti ya battery za Li-Po na Li-Ion.

Battery za Li-ion

Tofauti ya Battery za Simu Zenye Teknolojia ya Li-ion na Li-Po

Kama kawaida ya kipengele cha je wajua hua tunarudi nyuma kidogo kwenye historia. Battery za Li-ion au kwa kirefu Lithium-Ion Battery ziligundulika mwaka 1912, Battery hizi zilikuwa sio maarufu sana hadi pale kampuni ya Sony ilipo anza kuzitumia hapo mwaka 1991.

Sasa Battery hizi za Li-ion zina uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi chaji na pia hazina gharama kubwa kutengeneza.

Kingine ambacho ni tofauti kwenye Batter hizi ni kuwa, battery hizi zina tatizo la kuharibika kulingana na umri au muda, yani kadri miaka inavyozidi kwenda battery hizi zina uwezo wa kuharibika zenyewe, kifupi ni kuwa haziwezi kuishi kwa kipindi kirefu zikiwa na uwezo ule ule.

Sifa za Battery za Li-ion

  • Hali ya Hewa ya Kufanya Kazi – Battery hizi zinauwezo mzuri wa kufanya kazi kwenye hali ya hewa ya 4º F mpaka 140º F ( -20º C to 60º C)
  • Matumizi  – Battery hizi mara nyingi hutumika kwenye vifaa kama simu za mkononi kamera za kidigital pamoja na kompyuta za mkononi.
  • Maisha ya Battery – Battery hii inapoteza asilimia 0.1 kila mwezi mmoja.
  • Muundao – Kutokana na aina ya kemikali battery hizi huwezekana kuwa na muundao wa mstatili tu.
  • Usalama – Kutokana na kemikali battery hizi zikikaa kwenye joto au zikivuja huweza kulipuka kwa urahisi.

Battery za Li-Po

Tofauti ya Battery za Simu Zenye Teknolojia ya Li-ion na Li-Po

Kwa upande wa Battery za Li-Po au Lithium-Polymer Battery battery hizi ziligunduliwa mwaka 1970, battery ya kwanza kabisa kutengenezwa ya aina hii ilikuwa nyembamba kama vile line ya simu. Aina hii ya battery uwa na uwezo wa kutengenezwa zikiwa nyembamba sana na tofauti na battery za Li-ion battery hizi zina gharama kutengeneza na zinaweza kutengenezwa zikiwa nyepesi sana lakini zikawa na uwezo ulele wa kuhifadhi chaji.

Tatizo la battery hizi hua hazina uwezo wa kutunza chaji kwa muda mrefu kama zilivyo battery za Lithium-Ion Battery au Li-ion lakini pamoja na kwamba battery hizi hazidumu na chaji kwa muda mrefu sana, lakini pia battery hizi huwa na maisha mafupi zaidi ya battery za Li-ion.

Sifa za Battery za Li-Po

  • Hali ya Hewa ya Kufanya Kazi – Battery hizi zinauwezo mzuri wa kufanya kazi kwenye hali ya hewa ya joto au hata baridi.
  • Matumizi  – Battery hizi mara nyingi hutumika kwenye vifaa kama simu za mkononi kamera za kidigital pamoja na kompyuta za mkononi.
  • Maisha ya Battery – Battery hii aina maisha marefu kulinganisha na Li-ion
  • Muundao – Kutokana na aina ya kemikali battery hizi huwezekana kuwa na muundao wa tofauti kulingana na kifaa na pia battery hizi huwa nyembamba.
  • Usalama – Kutokana na hali ya hewa battery hizi mara nyingi ni vigumu kulipuka (ingawa zinaweza kulipuka) na pia huwa na uwezekano mdogo wa kuvuja.

Hitimisho

Kifupi ni kwamba kila battery hapa inayo faida na hasara yake na kwa upande wa kuwa na uwezo wa kudumu na chaji, hiyo uchochewa na aina ya kemikali battery iliyo tengenezewa hivyo battery za Li-po zinaweza kudumu na chaji zaidi kutokana na aina ya kemikali zilizo changanywa na vilevile hatua hiyo ni sawa pia kwenye battery za Li-ion.

Mpaka hapo natumaini utakuwa umepata ujuzi kidogo kuhusu tofauti za battery za Lithium-Ion au Li-ion pamoja na battery za Lithium-Polymer au Li-Po, kama utakuwa una maswali ushauri au hata kama kuna mahali utakua ujaelewa tupo kwaajili yako unaweza kuuliza swali lako hapo chini kwenye sehemu ya maoni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use