Tofauti Kati ya Simu za Tecno Camon X na Tecno Camon CM

Hii ndio tofauti iliyopo kati ya simu za Tecno Camon CM na Camon X
Tofauti kati ya Tecno Camon X na Camon CM Tofauti kati ya Tecno Camon X na Camon CM

Well.. moja kati ya simu ambazo zinatafutwa na watu wengi kwa sasa ni simu hizi mbili za Tecno Camon X na Tecno Camon CM. Simu hizi zinatafutwa kutokana na ubora wake pamoja na unafuu wake wa bei.

Pamoja na simu hizi zote kuwa za bei nafuu, lakini simu hizi zinakuja na utofauti ambao unafanya watu wengi kuchanganyikiwa na kushindwa kujua ni simu gani ya kuweza kununua. Sasa leo Tanzania Tech tunakusaidia kwenye hilo na tunaenda kuangalia tofauti kati ya simu hizi mbili ili kuweza kukusaidia kuchagua simu bora yenye kuendana na matumizi yako, Ni matumaini yangu mpaka mwisho wa makala hii utaweza kujua ni simu gani ununue, basi bila kupoteza muda twende tukangalie tofauti ya simu hizi.

Advertisement

  • Muundo

Kwa kuanza tuanze na muundo, Simu hizi za Tecno Camon X na Tecno Camon CM zinakuja na muundo unaofanana kwa muonekano lakini kuna utofauti kidogo kwenye simu hizi. Camon CM ni ndogo kidogo kuliko Camon X kwani Camon CM inakuja na ukubwa Inch 5.7 wakati Camon X yenyewe inakuja na ukubwa wa Inch 6. Vilevile Camon CM ni nyepesi kidogo kuliko Camon X, Camon CM inakuja na uzito wa 150g wakati Camon X inakuja na uzito wa 152g.

Kwa upande mwingine, Simu zote mbili zimetengenezwa kwa plastiki na zinakuja na muundo mzuri wa kujikunja kwenye kona (Curved Edge). Kwa upande mwingine Camon X inakuja na sehemu ya kuchomeka headphone kwa chini, wakati Camon CM inakuja na sehemu hiyo ya kuchomeka headphone kwa juu. Vilevile Camon CM inakuja na flash ambayo iko kwa chini ya kamera, wakati kwenye Camon X flash hiyo inapatikana kwa pembeni ya kamera. Simu zote mbili zinakuja na sehemu ya fingerprint inayopatikana kwa nyuma.

  • Sifa

Kwa upande wa sifa simu hizi zinakuja na utofauti kwa kiasi kikubwa kwani Camon X inakuja na RAM ya GB 3, wakati Camon CM inakuja na RAM ya GB 2. Kitu kingine ambacho ni tofauti kwenye simu hizi ni processor kwani Camon X inakuja na processor ya kubwa ya Octa-Core 2.0 GHz wakati Camon CM inakuja na Processor ya Quad-core 1.3 GHz.

Kwa upande wa ukubwa wa kioo, Camon X ina kioo cha inch 6.0 wakati Camon CM ina kioo cha inch 5.7, Vilevile uwezo wa Kioo cha Camon X na Camon CM ni sawa kwani simu zote zinakuja na vioo vyenye resolution ya 1440×720 pixel. Kwa upande mwingine simu hizi zinaendelea kufanana kwani simu zote mbili zinakuja na ukubwa wa ndani wa GB 16 kila moja.

  • Mfumo

Kwa upande wa mfumo wa uendeshaji, Tecno Camon X inakuja na mfumo wa Android 8.1 (Oreo) huku ikiwa na mfumo wa Tecno wa HiOS V3.3. Tecno Camon CM yenyewe inakuja na mfumo wa Android 7.0 (Nougat) huku ikiwa na mfumo wa Tecno HiOS 3.2.0.

Vilevile tofauti kubwa nyingine iliyoko kwenye simu hizi ni upande wa mfumo wa ulinzi wa Face ID kwani Tecno Camon X inakuja na mfumo huo wa kufungua simu kwa uso wakati Tecno Camon CM yenye haina mfumo huo.

  • Kamera ya Mbele

Kwa upande wa Kamera, Tukianza na Kamera ya mbele ya Camon X hii inauwezo mkubwa wa Megapixel 20 wakati kamera ya Camon CM yenyewe inakuja na uwezo wa Megapixel 13. Kwa muonekano wa picha hapo juu ni wazi simu ya Camon X inapiga picha za selfie vizuri kuliko kamera ya Camon CM na hii inachagiwa na ukubwa wa kamera hiyo ya Megapixel 20.

  • Kamera ya Nyuma

Kwa upande wa kamera za nyuma Camon X inakuja na Megapixel 16 wakati Camon CM inakuja na Kamera ya Megapixel 13. Lakini hata kwenye kamera za nyuma bado simu ya Camon X inaonekana ikiwa na picha zenye rangi angavu kuliko simu ya Tecno Camon CM.

  • Battery 

Kwa upande wa Battery bado Camon X inaendelea kuwa mbele kwa kuwa na Battery kubwa ya Li-ion yenye ukubwa wa 3750 mAh, wakati Camon CM yenyewe inakuja na Battery ya Li-ion yenye ukubwa wa 3000 mAh. Battery ya Tecno Camon X inaonekana kudumu na chaji zaidi kuliko Tecno Camon CM hiyo inatokana na ukubwa wa Battery yake hiyo.

Basi hiyo ndio tofauti liyopo kati ya simu hizi za Tecno Camon X pamoja na Tecno Camon CM, unaweza kuchunguza simu hizi zaidi kupitia maduka mbalimbali ya Tecno, kisha tuambie kwenye maoni hapo chini wewe umeonaje kuhusu tofauti kati ya Tecno Camon X pamoja na Camon CM. Kwa upande wangu naweza kusema, ni wazi kuwa Camon X ni simu nzuri kuwa nayo kama unataka simu yenye uwezo mzuri. Hata hivyo kama unataka kujua tofauti ya Tecno Camon X na Camon X Pro unaweza kusoma hapa kuweza kujua zaidi.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use