Kampuni ya Byte Dance kupitia app yake ya TikTok hivi karibuni imeanza majaribio ya video mpya ambazo zinasemekana kuwa na muda wa hadi dakika 3.
Kwa mujibu wa tovuti ya The verge, inasemekana watumiaji wataweza kuruhusiwa kurekodi au kuweka video zenye urefu wa hadi dakika 3 kwa kupitia toleo jipya la app ya TikTok au kwa kupitia tovuti ya tiktok.com.
Kwa sasa bado sehemu hiyo ipo kwenye majaribio kwa watu wachache, hadi hapo itakapo fanikiwa inaweza kuanza kufikia watu wengi zaidi.
Hadi sasa TikTok imeonekana kufanikiwa zaidi kwa kuruhusu video zisizo zidi dakika moja, huku wengi waki sema kuwa kuruhusu video za dakika tatu au zaidi kwenye mtandao huo kutafanya mtandao huo kukosa maana na kufanana na mitandao mingine kama YouTube ambapo video nyingi zina anzia dakika 3 na kuendelea.
Kuhusu sakata la TikTok kufungiwa nchini marekani, hivi karibuni kampuni ya ByteDance, ilipokea nyongeza ya siku saba zaidi ili kukamilisha kuuza shughuli zake kwa upande wa marekani. Hadi sasa bado haijajulikana kama kutokwepo madarakani kwa trump kunaweza kusaidia TikTok kuendelea na shughuli zake nchini humo kama awali.