Hatimaye kampuni ya TikTok imeweza kuepuka marufuku iliyokuwa iwekwe siku ya jumapili na idara ya biashara ya marekani, mara baada ya kampuni hiyo kufanikiwa kuingia mkataba na kampuni ya Oracle pamoja na kampuni ya Walmart.
Hata hivyo, kwa mujibu wa The Verge, marufuku hiyo ilikataliwa na mahakama ya marekani, mara baada ya kampuni ya TikTok kufungua kesi dhidi ya raisi Donald trump kusema kuwa, hatua ya kufungia app hiyo kunapinga uhuru wa kujieleza.
Hata hivyo, jaji Laurel Beeler wa Amerika alizuia marufuku hiyo, akisema inaibua maswali mazito juu ya katiba ya kwanza (ambayo inahakikishia uhuru wa kusema).
Mbali na hayo kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali inasemakana kuwa, Raisi wa marekani Donald Trump amekubali mkataba baina ya TikTok na kampuni hizo mbili, mkataba ambao utafanya kampuni mpya ya TikTok Global kuzaliwa.
Kampuni ya Oracle itakuwa na hisa asilimia 12.5%, huku kampuni ya Walmart ikiwa na hisa asilimia 7.5%. Hii inafanya kampuni mama ya TikTok, ByteDance kubaki na asilimia 80% ya hisa zote.
Mbali na hayo Wajumbe wanne kati ya watano wa bodi ya kampuni hiyo mpya watakuwa Wamarekani. Huku kampuni ya Oracle ikiwa na jukumu la kutoa huduma za uhifadhi salama, wakati Walmart itashughulikia vitu kama matangazo, malipo na kutimiza majukumu mengine.
Kulingana na taarifa ya Walmart, TikTok Global itaorodheshwa kwenye soko la hisa la Marekani “ndani ya miezi 12”., hii itasababisha kuongezeka kwa umiliki wa Marekani. Hata hivyo kampuni hiyo itakuwa na makao yake makuu nchini Marekani na itatengeneza ajira zaidi ya 25,000 nchini humo.
Hata hivyo, kampuni mama ya TikTok ByteDance ilisema kuwa haitahamisha teknolojia na algorithm yake kwa Oracle. badala yake, Oracle itaruhusiwa kukagua teknolojia hiyo ili kuhakikisha kuwa hakuna kitu chochote kinacho kikuka makubaliano hayo.