Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tigo Yashirikiana na Serikali Usajili wa Vyeti vya Kuzaliwa

Sasa usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto ni kupitia simu za mkononi
Cheti cha kuzaliwa Cheti cha kuzaliwa

Hivi karibuni Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Tigo imezindua usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambao utakuwa ukifanyika kwa kutumia simu za mkononi.

Katika kufanikisha mpango huo, Kampuni ya Tigo imetoa simu janja zaidi ya 900 zenye thamani ya Shilingi za kitanzania 95 milioni ili kuweza kufanikisha zoezi hilo kwa urahisi hapa Tanzania.

Advertisement

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo ya mawasiliano, Simon Karikari alisema kuwa kwa kupitia mpango huo Serikali inaweza kufuatilia usajili wa vizazi kwa urahisi zaidi kuanzia vijijini na kujua muda, mahali, umri hata jinsia ya kila mtoto anayesajiliwa kutoka popote nchini, hivyo kurahisisha matumizi ya taarifa hizi.

Karikari aliongeza kuwa umuhimu wa vyeti hivyo ni pamoja na kuwezesha kupata nyaraka nyingine za umma kama vile kitambulisho cha taifa, mpigakura, hati za kusafiria au leseni ya udereva na hata leseni za kampuni za biashara.

Aidha Mwenyekiti wa bodi ya Rita, Profesa Hamis Dihenga alisema kuwa utafika wakati itakuwa ni lazima kila mwananchi wa Tanzania kuwa na cheti cha kuzaliwa kwani hapo baadae hata kuanza shule kwa mtoto ni lazima cheti hiki kitahitajika ili watoto watambulike kwa urahisi alisema Profesa Dihenga.

Tayari mpango huo unaofadhiliwa na serikali ya Canada na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) unatekelezwa Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Songwe, Iringa, Geita na Njombe.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : Mwananchi

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use