Tigo Tanzania Yapunguza Gharama za Kutuma SMS na Kupiga Simu

Sasa utaweza kupiga simu kwa punguzo ya asilimia 27.5
Tigo Tanzania Tigo Tanzania

Hivi karibuni kampuni ya huduma za simu ya Tigo hapa Tanzania, imetangazwa kushusha gharama za kupiga simu pamoja na kutuma ujumbe mfupi ndani ya nchi na hata njie ya nchi.

Kupita takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kumekuwa na punguzo hilo katika robo ya nne ya mwaka iliyoishia Desemba 2017 ikilinganishwa na robo ya tatu ya mwaka ulioishia Septemba.

Advertisement

Kampuni ya Tigo imeonekana kupunguza gharama hizo kwa Asilimia 27.5, ambapo awali katika kupiga simu nje ya mtandao wateja wa Tigo walikuwa wakilipia Sh480 kwa dakika katika robo ya tatu ya mwaka ambayo imeshuka hadi kufikia Sh348 ambayo ni sawa na pungufu ya asilimia 27.5.

Kwa upande wa kupiga simu Afrika mashariki, wateja wa Tigo walikuwa wakilipia Sh1,022 kwa dakika katika robo ya tatu ya mwaka ambayo imepungua hadi kufikia Sh739 katika robo ya nne ya mwaka ikiwa ni pungufu ya Sh283 sawa na asilimia 27.7. Vilevile katika kupiga simu kimataifa, Tigo ilikuwa ikitoza Sh1,737 katika kupiga simu kwa dakika katika robo ya tatu ya mwaka ambayo imepungua hadi kufikia Sh1,258, ikiwa ni pungufu ya Sh479 sawa na asilimia 27.6.

Kwa upande wa kutuma ujumbe ndani ya mtandao, Kampuni ya Tigo imepunguza gharama hadi kufikia Sh51 katika robo ya nne ya mwaka kutoka Sh70 iliyokuwapo katika robo ya tatu ya mwaka, hiyo ni sawa na pungufu ya Sh19 sawa na asilimia 27.14. Kimataifa gharama pia zimepungua hadi kufikia Sh156 katika robo ya nne ya mwaka kutoka Sh 215 ya robo ya tatu ya mwaka ikiwa ni pungufu ya Sh59 sawa na asilimia 27.4.

Hii ni hatua ya kampuni ya Tigo kuelekea kwenye punguzo la gharama za kupiga simu ambapo, hivi karibuni TCRA ilitangaza kupunguza viwango vya gharama za mawasiliano ya simu kutoka shilingi 26.96 kwa dakika hadi shilingi 15.60 itakayoanza rasmi kutumiwa mwakani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use