Tigo Tanzania na Ericsson wameingia ubia ili kuzindua teknolojia ya 5G na kuboresha na kupanua mtandao wa 4G uliopo sasa nchini Tanzania.
Kwa sasa keknolojia ya 5G imezinduliwa na Tigo Tanzania kwenye mikoa ya Dar Es Salaam, Dodoma na Zanzibar na itaendelea kupelekwa kwa hatua katika maeneo muhimu kote nchini.
Ericsson kwa sasa inaboresha mtandao wa 4G wa Tigo Tanzania kwa kutumia teknolojia za Radio Access Network (RAN) pamoja na microwave (MINI-LINK 6000).
Kwa kutumia teknolojia hizi mtandao wa Tigo unapanuliwa na kuboreshwa zaidi na kuongeza uwezo wa mtandao.
Ericsson pia itaongeza ufanisi wa mtandao wa Tigo Tanzania kwa kuweka programu ya Cognitive Software yenye uwezo wa Artificial Intelligence (AI) ili kufikia malengo ya kimkakati ya utendaji wa mtandao.
Pia hii itasaidia kufanya utabiri wa kina wa mtandao ili kukidhi mahitaji ya utendaji yanayo ongezeka kila siku, pia kuboresha uzoefu wa mtumiaji.
Kamal Okba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo Tanzania, anasema: “Tumeshuhudia maendeleo makubwa hadi sasa; utendaji wa mtandao umepanda, na uzoefu wa wateja umeboreshwa sana kupitia uboreshaji na upanuzi wa mtandao wa 4G uliopo na uzinduzi wa 5G Dar Es Salaam, Dodoma, na Zanzibar.”
Binafsi nimeona mabadiliko makubwa ya mtandao wa Internet wa Tigo, kama upo Dar es salaam, Dodoma au Zanzibar je wewe umeona mabadiliko ya Internet kwenye mtandao wa Tigo..?