Kampuni ya huduma za simu ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Mastercard pamoja na Selcom imezindua rasmi kadi mtandao ya “Tigo Pesa Mastercard” ili kuwezesha malipo na manunuzi mtandaoni.
Akizungumza na waandishi wa habari Machi 21, 2023 jijini Dar es Salaam Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema kuwa huduma hiyo ni muendelezo wa kuwarahisishia wateja wao kuendelea kuishi maisha ya kidigitali kwa kufanya manunuzi mtandaoni.
Kwa sasa kampuni ya Tigo ni miongoni mwa kampuni nyingine kama Vodacom, na Airtel ambazo nazo zinatoa huduma hii ya manunuzi kupitia huduma za kifedha kupitia simu.
TABLE OF CONTENTS
Aina za Tigo Pesa Mastercard
Kwa sasa Tigo Pesa Mastercard inakuja na aina mbili za kadi. Kama kwa namna yoyote unataka kujiunga na Tigo Pesa Mastercard kwa ajili ya kufanya manunuzi mtandaoni basi ni vyema ufahamu kuwa Tofauti na mitandao mingine Tigo Pesa Mastercard inakuja na aina mbili za kadi.
Kadi ya kutumika kwa siku tisini, pamoja na kadi ya kutumika kwa siku saba. Kadi hizi zote zina utafauti kulingana na matumizi yako.
Kadi ya Siku 90
Tigo Pesa Mastercard kadi ya siku tisini 90 hii hutumika kwa muda wa siku 90 na inaisha muda wake ndani ya siku hizo hadi pale mtumiaji atakapo tengeneza upya na kuendelea kutumia, au kafuta pale ambapo haitaji kutumia.
Kadi ya Mara Moja
Kadi ya mara moja hii ni kadi ya Tigo Pesa Mastercard ambayo hutumika ndani ya muda maalum ambao utakuwa umechagua na kadi hii uweka kiasi cha pesa kulingana na matumizi. Kadi hii hufanya kazi kwa muda mfupi na huwezi kurenew ili kuendelea kutumia na pia kadi hii huifadhi pesa kulingana na huduma unayotaka kulipia na sio zaidi.
Jinsi ya Kutengeneza Tigo Pesa Mastercard USSD
Kama unataka kutengeneza, Tigo Pesa Mastercard unaweza kufuata hatua zifuatazo, kitu cha muhimu hakikisha ume wezeshwa na huduma za Tigo Pesa ili kuendelea.
Hatua ya Kwanza bofya Menu ya Tigo Pesa *150*01#, Kisha chagua namba 7 ambayo ni huduma za kifedha.
Baada ya hapo kwenye menu inayofuata unatakiwa kubofya namba saba 7 ambayo ni Menu ya Tigo Pesa Kadi.
Baada ya hapo utapelekwa kwenye Menu kuu ya Tigo Pesa Mastercard na moja kwa moja unatakiwa kubofya namba 1 kutengeneza kadi.
Baada ya hapo utakaiwa kusoma vigezo na masharti na kukubali, kama unataka kusoma vigezo hivyo unaweza kutembelea www.t&c.co.tz/vcn. Kwenye hatua hizi unatakiwa kubofya 1 kuendelea kama umekubali vigezo na masharti ya matumizi.
Baada ya hapo unatakiwa kuchagua aina ya kadi unayotaka, kama unataka kadi ya siku 90 ambayo hii inaweza kuendelea kutumika baada ya kurenew baada ya kuisha muda wake unaweza kuchagua namba 2.
Kama unataka kadi ya kutumia mara moja ambayo hii uwezi kurenew na pia inatumika kwa kiwango maalum cha pesa basi chagua namba 1.
Baada ya hapo kama unachagua namba moja 1 ambayo ni kadi ya matumizi ya mara moja unatakiwa kuweka kiwango unachotaka kutumia kwenye kadi hiyo, na kadi hiyo hitoweza kufanya miamala zaidi ya kiwango ulicho chagua kwenye hatua hii.
Kama utachagua namba mbili moja kwa moja utaweza kutumiwa taarifa za kadi ambazo hizo ndio utatumia kuweza kufanya manunuzi na kulipia huduma mbalimbali mtandaoni.
Tengeneza Tigo Pesa Mastercard Kwa Kutumia Tigo Pesa App
Pia unaweza kutengeneza Tigo Pesa Mastercard Kwa Kutumia Tigo Pesa App, unaweza kufanya hatua hizi moja kwa moja kwa kupakua app ya Tigo Pesa app kama bado huna app hiyo kisha endelea kwenye hatua kwenye video hapo chini.
Tigo Pesa App Android
Tigo Pesa App iOS
Baada ya kupakua app moja kwa moja unaweza kufuata hatua hizi rahisi (Kupitia Video Hapo chini) kupitia app ya Tigo Pesa App moja kwa moja.
Hitimisho
Kwa kufanya hatua hizo utakuwa umeweza kutengeneza Tigo Pesa Mastercard na utaweza kulipia huduma mbalimbali mtandaoni kama vile kuafanya manunuzi mtandaoni, kulipia huduma za Netflix, Kufanya matangazo Instagram, Facebook pamoja na huduma nyingine zote za muhimu.