Ni wazi kuwa mawasiliano ni kitu cha msingi sana, lakini je inakuaje pale mtandao unapokuwa haupo au pale inapotokea kukatika kwa mawasiliano ya minara ya simu kutokana na sababu mbalimbali kama vile maafa na mambo mengine kama hayo..?
Thuraya X5-Touch ni simu ya kwanza ya android kuwa na uwezo wa Satellite, simu hii inauwezo wa kufanya kazi kama simu janja ya kawaida ya Android na pia inauwezo wa kufanya kazi kama Simu inayotumia Satellite. Thuraya X5-Touch inakuja na kioo cha IPS Display chenye inch 5.2 pamoja na resolution ya 1080 Pixel.
Japo kuwa simu hii imepewa taji la kuwa simu ya kwanza ya Android yenye Satellite, kwa upande wa sifa bado ni simu yenye sifa za kawaida sana. Simu hii inatumia processor ya Snapdragon 625 chipset ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16. Simu hii pia inatumia Mfumo wa uendeshaji wa zamani kidogo wa Android 7.1 Nougat.
Thuraya X5-Touch pia inakuja na kamera za Megapixel 2 kwa mbele na kwa nyuma inakuja na kamera ya Megapixel 8. Simu hii inaendeshwa na battery yenye uwezo wa 3800 mAh ambayo ukichanganya na utumiaji wa Satellite inaweza kuduma kwa muda wa masaa 23 au siku moja nzima lakini yote inategemeana na matumizi yako.
Simu hii inakuja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi IP67 na pia imepewa kibali cha MIL-STD-810 kwa kuwa simu yenyewe uwezo wa kuimili mazingira magumu. Thuraya X5-Touch pia inakuja na teknolojia za NFC pamoja na teknolojia za ramani za GPS, BeiDou, na GLONASS. Simu hii inatumia line mbili na inauwezo wa internet wa 4G, 3G pamoja na 2G.
Thuraya X5-Touch inategemewa kupatikana kwenye inchi 160 duniani na bei yake itakuwa inaanzia Euro £999 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 2,950,000 bila kodi.
Nimependa sana uduma zenu zimetufungua macho.