Kama wewe ni mmoja wa watu ambao umeshawahi kufanya malipo ya serikali, kama vile Luku, Bili ya maji au kodi mbalimbali za TRA basi makala hii inakuhusu.
Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi sana ambayo unaweza kutumia kuthibitisha malipo mbalimbali, hii ikiwa na maana kuwa, kama kuna mtu amenunua umeme na huna uhakika kama amenunua basi njia hii inaweza kukusaidia.
Au hata kama umepoteza namba za Luku au unataka tu kuthibitisha kama malipo yamefanyika kwa usahihi basi makala hii itakusaidia sana. Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi twende kwenye makala hii.
Kwa kuanza ingia kwenye soko la Play Store kisha pakua app ya GePG Tanzania, app hii ni official app ya mfumo wa malipo ya serikali na itakusaidia sana kuthibisha malipo ikiwa pamoja na kufanya malipo mbalimbali ya serikali kama vile Faini, Kodi, Bili za Serikali na mengine mengi.
Baada ya kownload na kuinstall vizuri kwenye simu yako sasa endelea kwa kufungua app hiyo.
Moja kwa moja utaweza kuona mfumo huu na sasa kama unataka kudhibitsha malipo sasa endelea kwa kuchagua sehemu ya Verify Payment. Baada ya hapo chagua njia ya kuthibitisha, unaweza kuchagua njia ya kuthibitisha kwa Control Number, Bank Receipt au kwa GePG Receipt.
Njia hii ni bora kama unataka kuthibitisha malipo ya Maji, au malipo mbalimbali ya serikali ambayo hupokelewa kwa kutumia Control namba. Yani hii ni njia bora kama malipo uliyoya fanya ulitumia Control namba.
Kama unataka kuthibitisha malipo ya LUKU basi moja kwa moja chagua sehemu ya LUKU kisha bofya Get last tokens. Hii itakusaidia kujua kiwango cha mwisho cha umeme ulio wekwa kwenye mita yako ya LUKU.
Baada ya kuchagua Get last token, sasa endelea kwa kuchagua sehemu njia ya kupata token hizo, kuna njia nne lakini njia ambayo ni rahisi zaidi ni njia ya kutumia Meter Number kwa sababu pale unatumia njia ya namba ya simu mtu anaweza kukwambia labda alinunua umeme kwa kutumia namba nyingine ya simu.
Baada ya kuchagua Meter Number sasa ingiza namba za mita na moja kwa moja utaweza kuona kiasi kilichowekwa ikiwa pamoja na tarehe ya malipo pamoja na token namba zilizowekwa. Hii inaweza pia kukusaidia kama umenunua umeme na kwa bahati mbaya haujatumwa kwenye simu yako au umechelewa kuja.
Pia kupitia app hii utaweza kufanya malipo mbalimbali kwa haraka na kwa urahisi na kutokana na kuwa app hii imeunganishwa na mfumo wa malipo hayo ya Serikali basi malipo yanafanyika moja kwa moja kwa urahisi na haraka.
Hadi hapo natumaini hii inaweza kukusaidia kwenye hali mbalimbali, kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Pia unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kurudisha SMS zilizo futika kwenye simu yako ikiwa na njia ya kufanya back ya SMS zako.