Kampuni ya Apple ipo mbioni kufanya mkutano wake wa kila mwaka unaojulikana kama WWDC au Apple Worldwide Developers Conference, mkutano huu uhusisha wabunifu mbalimbali wa programu na bidhaa za Apple na mara nyingi kwenye mkutano huu Apple huonyesha bidhaa mpya pamoja na maboresho ya bidhaa zake za awali.
Moja ya maboresho yanayo tarajiwa siku za karibuni ni pamoja na Programu ya siri kuongezewa sauti mpya. Kwa mujibu wa tovuti ya The next web, Programu ya siri yenyewe ndio imetoa siri hiyo, na unaweza kujaribu kama unatumia simu ya iPhone au iPad yenye uwezo wa programu ya Siri, unaweza kuuliza programu hiyo kwa kusema “Tell Me About WWDC”.
Mbali na hayo inawezekana kuwa Apple itazindua spika janja mpya kwenye mkutano wa WWDC, simu mpya ya iPhone SE 2, pamoja na mambo mengine mengi kuhusu mfumo mpya wa uendeshaji wa iOS na MacOS. Endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha yote yatakayojiri kwenye mkutano huo unaotarajiwa kuanzia rasmi tarehe 4, mwezi wa sita 2018, hadi tarehe 8 June 2018.