Baada ya Kampuni ya Tecno kuzindua simu mpya ya Tecno Camon CM, Tetesi zinasema kuwa kampuni ya Tecno sasa inajiandaa kuja na toleo jipya la simu ya Tecno Camon X (2018), inayo tarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi ujao. Toleo hilo jipya la Tecno Camon X litakuja likiwa na uwezo na sifa makini zaidi tofauti na toleo la mwaka jana la Camon CX.
Habari kutoka tovuti ya techweez zinasema kuwa, toleo hilo jipya linakuja likiwa limeangazia zaidi kwenye upande wa picha na litakuja likiwa na maboresho zaidi hasa kwa upande wa kamera. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, simu hiyo ya Camon X inatarajiwa kuja na kamera kubwa ya nyuma yenye uwezo wa Megapixel 60 pamoja na kamera mbili za mbele.
Bado haijajulikana zaidi kuhusu sifa kamili za simu hiyo, lakini tetesi zinadai kuwa simu hiyo itakuja na teknlojia mpya ya mfumo wa kupooza simu pamoja na sifa zingine kama RAM ya ukubwa wa kati ya GB 4 au GB 6, ukubwa wa ndani hadi GB 128 pamoja na mfumo wa uendeshaji wa Android 8 Oreo.
Tetesi hizo pia zinadai kuwa simu hizo zitakuja za aina mbili ambazo zitakuwa Tecno Camon X pamoja na Tecno Camon X Pro, ambapo toleo la Pro linasemekana kuja na uwezo mkubwa wa RAM pamoja na ukubwa wa ndani mkubwa zaidi. Hata hivyo ripoti hizo zinadai kuwa simu hizo zinategemewa kuzinduliwa mwezi wa nne na inasemekana usinduzi utanyika rasmi nchini Nigeria.