Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tetesi : Hii Hapa Picha ya Kwanza ya Muonekano wa Galaxy Note 9

Simu hii inasemekana kuwa itakuja na Fingerprint kwenye kioo
Galaxy Note 9 Galaxy Note 9

Imebaki miezi michache mpaka kampuni ya Samsung kurudi na toleo la tisa la simu yake ya Samsung Galaxy Note 9, wakati tukiwa tunasubiri simu hiyo tayari kumesha zuka tetesi mbalimbali zenye kuonyesha baadhi ya vitu vinavyo tarajiwa kuwepo kwenye simu hiyo. Moja kati ya tetesi ambazo nimeona nikusogezee siku ya leo, ni hii ya picha ya muonekano wa simu hiyo ya Galaxy Note 9.

UpdateBaada ya kuzinduliwa rasmi kwa Galaxy Note 9, Hizi Hapa ndio picha halisi na sifa za simu hiyo.

Advertisement

Hapo chini ni picha inayosemekana kuwa ndio yenye muonekano halisi wa simu ya Galaxy Note 9, Picha hiyo imetoka kwenye ukurasa wa Twitter wa mvujishaji maarufu wa nchini china anaejulikana kama Ice universe.

Bado hakuna taarifa kamili kama hii ndio picha halisi ya simu hiyo, lakini kwa mujibu wa mvujishaji huyo, Samsung Galaxy Note 9 itakuwa haina tofauti sana na Galaxy Note 8 na kwa upande wa muundo pia simu hii inasemekana kuwa itakuwa na muundo ule ule kama wa Galaxy Note 8. Hata hivyo kwa mujibu wa tetesi nyingine inasemekana pia Galaxy Note 9 itakuwa ndio simu ya kwanza kutoka kampuni ya Samsung ambayo itakuja na sehemu ya Fingerprint kwenye kioo.

Kwa upande mwingine wataalam wa maswala ya teknolojia wanasema kuwa simu hiyo itakuwa haina tofauti sana na Note 8 lakini inategemewa kuja na maboresho mengi kwa upande wa mfumo wa uendeshaji, ikiwa pamoja na kamera za simu hiyo hasa zile za nyuma ambazo zinategemewa kuja mbili kwa nyuma.

Kwa mtazamo huo je vipi unasemaje kuhusu muonekana wa simu hiyo..? Je nini ungependa kuona kwenye simu hiyo mpya ya Galaxy Note 9, tuambie kwenye maoni hapo chini.

2 comments
    1. Hii inategemeana na mahali na pia sababu nyingine ni kutokana na ujio wa Galaxy S9 na Galaxy Note 9.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use