Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy A60

Sifa za Galaxy A60 zimevuja kabla ya simu hiyo kutoka rasmi
Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy A60 Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy A60

Kampuni ya Samsung bado inaendelea kuja na simu zake mpya za Galaxy A za mwaka 2019, kama umegundua mwaka huu kampuni hiyo inakuja na simu hizi zikiwa na majina ya tofauti na hapo awali. Kwa mfano sasa kuna Galaxy A50 na Galaxy A30 na sasa jiande kuipokea Galaxy A60.

Sasa kwa upande wa Galaxy A60 yenyewe inatarajiwa kuwa simu ya kisasa zaidi huku ikiwa na sifa bora zaidi. Kwa mujibu wa tetesi zilizo sambaa kupitia tovuti ya slashleaks, Galaxy A60 inatagemewa kutoka siku za karibuni huku ikiwa na sifa kama zifuatazo.

Advertisement

Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Samsung Galaxy A60

Kama unavyoweza kuona hapo juu, Galaxy A60 inatarajiwa kuwa na kamera tatu moja ikiwa na Megapixel 32 na nyngine ikiwa na Megapixel 5 na ya mwisho ikiwa na Megapixel 8. Kwa upande wa Selfie simu hii pia inaonekana kuja na kamera ya Selfie ya Megapixel 32. Mbali na hayo simu hii inaonekana kuendeshwa na processor ya Snapdragon 6150 chipset huku ikisaidiwa na RAM ya GB 6 au GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128.

Vilevile inaonekana simu hii itakuja na sehemu ya Fingerprint iliyopo chini ya kioo, huku simu hiyo ikiendeshwa na battery kubwa yenye uwezo wa 4500mAh.

Kama unavyoweza kuona simu hii inakuja na kamera kubwa kuliko hata Samsung Galaxy S10 ambayo imezinduliwa hivi karibuni. Bila shaka samsung imeanza kufanyia kazi ile kauli ya mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya hiyo Dj Koh, aliposema kuwa “Kwa sasa kampuni ya Samsung inangalia zaidi simu za daraja la kati (Mid-Range), kuliko simu za daraja la juu (Flagship)”.

Kwa sasa bado haijajulikana lini simu hii itatoka rasmi, lakini tegemea kuona simu hii ndani ya kipindi cha miezi hii miwili kuanzia sasa. Kupata taarifa zaidi kuhusu simu hii pamoja na kujua sifa zake kamili endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use