Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tetesi : Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Galaxy Note 20

Muonekano wa kwanza wa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 20
Tetesi : Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Galaxy Note 20 Tetesi : Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Galaxy Note 20

Wakati ikiwa imebaki miezi michache hadi kampuni ya Samsung kuzindua simu mpya ya Galaxy Note 20, hivi karibuni tayari tetesi zimeanza kusambaa mtandaoni zikionyesha muonekano wa simu hiyo mpya kutoka Samsung.

Kwa mujibu wa tovuti ya 9to5google, Galaxy Note 20 inatarajiwa kuzinduliwa mwezi wa nane mwaka huu 2020, ambapo inasemekana kuwa tamasha la uzinduzi wa simu hiyo linategemea kufanyika mtandaoni, hii ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kutoka kwa simu hizo. Hata hivyo inasemekana kuwa sababu ya kufanya tamasha hilo ikiwa ni kuepuka msongamano kutokana na maambukizi ya virusi vya corona yanayo sababisha ugonjwa wa COVID-19.

Advertisement

Tetesi : Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Galaxy Note 20
Mbali na hayo kwa mujibu wa tetesi zinazo sambaa kutoka tovuti mbalimbali mtandaoni, inasemekana kuwa picha hapo juu ndio inayo onyesha muonekano halisi wa simu mpya ya Galaxy Note 20 ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwezi wa nane mwaka huu 2020.

Kwa mujibu wa picha hiyo, inasemekana kuwa kwa nyuma Galaxy Note 20 itakuja na muonekano unaofanana kidogo na simu mpya ya Samsung Galaxy S20 Ultra ambayo inakuja na kamera za nyuma zikiwa kwenye mzunguko maalum kama inavyo onekana kwenye picha ya hapo chini.

Tetesi : Picha za Muonekano wa Simu Mpya ya Galaxy Note 20
Mbali na hayo, inasemekana kuwa simu hiyo itakuwa na kioo kikubwa cha inch 6.9 huku ikiwa na camera ya selfie ambayo itakuwa juu ya kioo kama zilivyo simu za Galaxy S20. Kamera hiyo inategemewa kuwa na uwezo mkubwa huku ikiwezeshwa na teknolojia mbalimbali kama Artificial Intelligence au AI na Face Unlock pamoja na teknolojia nyingine zitakazo kusaidia kupiga picha za selfie zenye muonekano bora.

Hata hivyo mbali na picha hiyo, ipo video ambayo imetengenezwa ikiwa ina onyesha muonekano wa simu hiyo kwa kuzingatia tetesi hizo. Unaweza kuangalia video hapo chini ila kumbuka hizi ni tetesi za awali za muonekano wa simu hiyo, mengi yanaweza kubadilika kadri muda wa uzinduzi wa simu (mwezi wa nane mwaka huu 2020) hiyo unavyozidi kukaribia.

2 comments
  1. Habari za muda huu kiongozi wangu.

    Mimi ni mtunzi wa mashairi, tenzi, riwaya na kadhalika.
    Hivi karibuni nimeanzisha blog yangu ila bado ni changa

    LAKINI

    Nahitaji kuitangaza blog yangu katika blog yenu hii je gharama ziko vipi?

    Blog yangu ni
    www.mrbunduki.com

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use