Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei Mbioni Kuanza Kutumika

Huenda mfumo huo ukawa tayari kwa matumizi kati ya mwaka huu 2019 na mwaka 2020
Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei Mbioni Kuanza Kutumika Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei Mbioni Kuanza Kutumika

Habari mpya hivi karibuni zinasema kuwa, Kampuni ya Huawei inategemea kuanza kutumia mfumo wake wa uendeshaji ambao utakuwa unafanya kazi kama mfumo wa Android.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya TechRadar, mfumo huo ambao kwa sasa unajulikana kwa jina la HongMeng, umeanza kufanyiwa kazi na kampuni ya Huawei hata kabla ya kampuni hiyo kufungiwa kufanya biashara na kampuni yoyote ya marekani. Techradar imeeleza kuwa, mfumo huo unasemekana ulikuwa umekamilika tangu January mwaka jana 2018.

Advertisement

Hata hivyo inasemekana mfumo huo wa Hongmeng OS utakuwa unafanyakazi sawa na mfumo wa Android, huku pia programu (Apps) zote za Android zikisemekana kuwa na uwezo wa kupakuliwa na kuwa installed kwenye simu inayotumia mfumo huo kutoka Huawei.

Bado hakuna tetesi zozote kuhusu muonekano wa mfumo huo, ila TechRadar imeandika kuwa, msemaji wa Huawei amesema huwenda mfumo huo uka anza kutumika kuanzia mwishoni mwa mwaka huu 2019 huko nchini China, na baadae mwaka 2020 kuanza kutumika dunia nzima.

Hatua hii inakuja siku chache baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei, Ren Zhengfei kusema kwa ujasiri kuwa, pamoja na vikwanzo vya Marekani hakuna mtu anayeweza ‘kuikamata’ Huawei katika kipindi cha miaka miwili au mitatu ijayo, kwani kama kampuni binafsi inauwezo wa kutoa faida zaidi kwa sababu inaweza kufanya uwekezaji mkubwa kwa urahisi zaidi.

Pamoja na yote hayo bado hakuna anaye weza kujua moja kwa moja mipango ya baadae ya kampuni ya Huawei, hivyo ni wazi tunahitaji kuendelea kufuatailia mabadiliko haya ya Huawei ili kuweza kujua zaidi.

Kwa habari zaidi hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku, pia hakikisha una subscribe kwenye channel yetu ambapo utaweza kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use