Tetesi Kuhusu Toleo Jipya la Playstation 4K

Tetesi Kuhusu Toleo Jipya la Playstation 4K Tetesi Kuhusu Toleo Jipya la Playstation 4K

Tetesi zinazoendela kote duniani kuhusu Playstation 4 zinasema kuwa huenda kampuni ya Sony ikatoa toleo jipya la Playstation 4 ambalo litakuwa limeongezewa baadhi ya vitu kama vile CPU pamoja na RAM. Hata hivyo blog mbalimbali za habari za teknolojia zimeonekana kutoa ripoti hizo kuwa Playstation hiyo mpya itakuja na jina la kitaalam (Codename) lijulikanalo kama “NEO”, imeandika moja ya blog hizo za habari za teknolojia ijulikanayo kama Giant Bomb.

Hata hivyo Blog hiyo maarufu imeendela kuandika kuwa Playstation ya octocore au ‘Jaguar’ iliyopo sasa itaongezewa uwezo wa CPU kutoka 1.6GHz mpaka 2.1GHz, pia GPU itaongezwa kutoka 18 compute units 800MHz  mpaka 36 compute units 911MHz memory card itabakia kuwa GB8 lakini itaongezewa speed kutoka 176GB/s mpaka 218GB/s. Kuongezwa huku kutawezesha Playstation hiyo kuwa na uwezo wa kusoma video pamoja na game za teknolojia ya 4K pamoja na kutimiza maitaji ya kutumia Playstation VR ambayo ilitangazwa kutoka hivi karibuni.

Advertisement

Giant Bomb iliendela kuandika kuwa kiasi cha hard disk kinategemewa kuwa kama ilivyokua hapo awali yani GB500 lakini haijajulikana kikamilifu kama itakua katika upande wa hard disk au network connection illiandika blog hiyo siku ya tarehe 18 march 2016. Hata hivyo watu wengi duniani wameonekana kutoku furahishwa na jambo hili ikitegemewa wapenzi wa game hizo wamekua wakitoa maoni mbalimbali kuhusu kuongezwa kwa ukubwa wa hard disk ya game hizo. Hata hivyo sony haijasema lolote kuhusiana na tetesi hizo za kutoka kwa game hiyo ya Playstation NEO au PS4K.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use