Kampuni ya Huawei inajiandaa kuja na simu yake mpya ya Huawei Nova 3, simu hii inatarajiwa kuja rasmi tarehe 18 mwezi huu huku ikiwa na maboresho makubwa ya toleo la mwaka jana la Huawei Nova 2. Hata hivyo, wakati tukiwa bado tunasubiri kuzinduliwa rasmi kwa simu hiyo, tayari kumeshavuja picha zenye muonekano halisi wa simu hii.
Simu hii ya Huawei Nova 3 inakuja na processor ya octa-core CPU, yenye speed ya 2.3 GHz ambayo itakuwa ikisaidia wa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128. Huawei Nova 3 pia inakuja na kioo cha HD LCD cha inch 6.3 chenye aspect ratio ya 19.9 na dimension ya 157 x 73.7 x 7.3 mm na uzito wa gramu 166.
Vilevile simu hii inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa 3,750 mAh huku ikiwa na teknolojia ya Super Charge by Huawei inayoweza kuchaji simu hiyo kwa haraka zaidi. Kamera za simu hii zinakuja mbili kwa nyuma ikiwa moja inauwezo wa Megapixel 16 na nyingine Megapixel 24 huku kwa mbele pia ikiwa na kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 24 na nyingine ikiwa na Megapixel 2.
Simu hii pia inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Android 8.0 huku ikiwa na mfumo wa Huawei EMUI 8.3 pamoja na programu mbalimbali maalum za 3D Qmoji, mfumo wa AI au Artificial intelligence na mambo mengine mbalimbali. Kwa sasa simu hii bado haijazinduliwa rasmi hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech kujua sifa nyingine kamili za simu hii.