Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Galaxy S21 Mapema (2021)

Tegemea kupata simu hii mpya pamema mwezi January mwaka 2021
Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Galaxy S21 Mapema (2021) Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Galaxy S21 Mapema (2021)

Wakati ikiwa taratibu tunasogelea mwisho wa mwaka 2020, kampuni ya Samsung hivi karibuni inatarajiwa kuzindua simu yake mpya ya Galaxy S21. Pengine unajiuliza hivi karibuni ni lini.?

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali inasemekana kuwa simu mpya ya Galaxy S21 inatarajiwa kuja mapema kuliko ambavyo imezoeleka. Inasemekana kuwa simu hii inatarajiwa kuja kwa matoleo matatu, toleo la Galaxy S21, Galaxy S21 Plus na Galaxy S21 Ultra.

Advertisement

Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Galaxy S21 Mapema (2021)

Kwa upande wa kioo, Galaxy S21 itakuwa na kioo cha inch 6.2 huku zote pia zikiwa na teknolojia ya FHD+ pamoja na 120Hz refresh rate. Kwa upande wa S21 Plus itakuja na kioo cha inch 6.7 huku S21 Ultra ikija na kioo cha inch 6.8.

Kwa upande wa Galaxy S21 Ultra simu hii ndio inasemekana kuja na uwezo zaidi huku ikiwa inakuja na kalamu maalum ambayo hii tumesha zoea kuiona kwenye simu za Galaxy Note. Hata hivyo tetesi zinasema kuwa mwaka 2021 inawezekana Samsung isizindue simu mpya za Galaxy Note kama ilivyo zoeleka, lakini tufanye hii ni mada ya siku nyingine.

Tetesi : Jiandae na Simu Mpya ya Galaxy S21 Mapema (2021)

Kama unavyoweza kuona picha hapo juu, hiyo ni picha halisi ya Galaxy S21 Ultra ambayo pia inakuja na kalamu maalum.

Mbali na hayo kitu kingine ni upande wa kamera, Simu hizi zinakuja na kamera ambazo karibia zinafanana huku S21 Ultra ikiwa na kamera nne tofauti na S21 na S21 Plus ambazo zinakuja na kamera tatu kwa nyuma.

Kwa upande wa battery inasemekana kuwa S21 itakuja na uwezo wa battery ya (4,000 mAh), Galaxy S21 Ultra (5,000 mAh), wakati Galaxy S21+ (Plus) ikiwa inasemekana kuja na uwezo wa battery ya 4,800 mAh. Simu zote zinakuja na teknolojia ya Fast Charging.

Kwa upande wa upatikanaji, Simu zote za Galaxy S21 zinatarajiwa kuzinduliwa mapema tarehe 14 mwezi January mwaka 2021, ikiwa ni takribani siku 43 kuanzia leo tarehe 17 mwezi huu wa kumi na moja mwaka 2020.

Kujua zaidi kuhusu simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tutakuletea habari zote  kuhusu simu hii na nyingine nyingi. Kujua zaidi kuhusu sifa na bei ya simu mpya unaweza kutembelea tovuti yetu ya Price in Tanzania hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use