Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Hatua ya kwanza hadi ya mwisho jinsi ya kutengeneza website ya muziki
Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure) Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania tech basi najua unajua kuwa siku kadhaa zilizopita tuli onyesha jinsi ya kutengeneza website ya nyimbo mpya au muziki kwa kutumia smartphone, njia hizo zilikuwa zipo kwenye awamu mbili, awamu ya kwanza ilikuwa ni kuweka website yenyewe kwenye server ya bure, na awamu ya pili ilikuwa ni jinsi ya kupata domain ya bure.

Kwa siku ya leo nitamalizia sehemu ya tatu ambayo ni ya mwisho ikiwa pamoja na kuonyesha baadhi ya njia ambazo unaweza kutumia kutatua matatizo mbalimbali ambayo nimeona wengi wenu mnakutana nayo.

Advertisement

Kwa kuanza kama wewe ni mgeni unaweza kuanza kwa kuangalia video hizi mbili ambazo zimeonyesha vizuri jinsi unavyoweza kuanza kutengeneza website hiyo ya nyimbo mpya kwa kutumia smartphone yako.

Kuweka File za Tovuti

Kwenye awamu hii ya kwanza mambo unayo hitaji ni machache sana, kama nilivyo ainisha kwenye video unahitaji kuwa na akaunti ya Google, unahitaji kutengeneza akaunti kupitia tovuti ya infinityfree (nimeonyesha hatua zote hapo juu), na mwisho unahitaji kupakua file la Muziki ambalo ndio linakuja na code za muhimu za website yenyewe ya muziki au nyimbo mpya.

Unaweza kupata link zote za muhimu kupitia hapa chini hivyo hakikisha una angalia video hiyo hatua kwa hatu kisha utaweza kuendelea kwenye awamu ya pili bila tatizo lolote.

1. Download File la MUZIKI Hapa

2. Tovuti ya Infinityfree Hapa

3. Pia unaweza kutumia Hosting ya Bure Hapa

4. Tembelea tovuti ya Google kupata YouTube API

Link hizo hapo juu zinatosha kabisa kusaidia kumaliza awamu ya kwanza na moja kwa moja twende tuka angalie awamu ya pili ambayo ilikua ni jinsi ya kupata domain ya bure ikiwa pamoja na kuiweka kwenye website yenyewe.

Kuweka Domain

Kwenye awamu hii unatakiwa pia kuangalia video hiyo kwa makini, kama ilivyo awamu ya kwanza kuna baadhi ya vitu vichache ambavyo utakuwa unahitaji ili kuweza kupita kwenye hatua hii.

Vitu hivyo ni pamoja na akaunti ya freenom, pamoja na akaunti yako ya infinity free ambayo tulitengeneza kwenye awamu ya kwanza, Kumbuka njia hizi zinategemeana hivyo ni muhimu kuangalia video ya kwanza ndipo uweze kuendelea kwa kuangalia video hiyo.

Unaweza kupata link zote za muhimu ambazo zimetajwa kwenye video hii, kumbuka akaunti yako ya freenom inatakiwa kusajiliwa kwa ukamilifu kabla ya kuanza kutumia domain za bure. Pia kumbuka ni muhimu kuchagua domain ya .ML na sio .TK au domain nyingine.

1. Tovuti ya Freenom hapa kwa ajili ya Domain ya bure

3. Tembelea Tovuti ya infinity free hapa

Baada ya kufanya hatua zote hizi kwa usahihi basi sasa upo tayari kuendelea kwenye hatua ya tatu na ya mwisho ambayo ni jinsi ya kubadilisha jina pamoja na kuweka matangazo kwa ajili ya kupata kipato kutoka na tovuti hiyo.

Kubadili Jina na Kuweka Matangazo

Awamu hii ndio awamu ya mwisho ambayo ndio inafunga ukurasa mzima wa njia hii ambayo tumekuwa nayo kwa muda wa mwezi mzima hadi sasa, kupitia hapa nitaenda kuonyesha njia rahisi ya kubadilisha jina pamoja na kuweka matangazo yanayolipa zaidi ya matangazo ya Google Adsense.

Kubadili Jina

Kwa kuanza labda tuanza na jinsi ya kubadilisha jina la website, ndani ya file zile ambazo tuliziweka kwenye server unatakiwa kuingia kwa kupitia akaunti yako ya infinityfree Kisha baada ya hapo bofya akaunti yako alafu bofya sehemu ya File Manager.

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Baada ya kubofya sehemu ya file Manager subiri kidogo utapelekwa kwenye sehemu ambayo uliweka file zako za tovuti yako.

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Baada ya sehemu hiyo kufunguka, chagua kwa kubofya sehemu ya htdocs kisha chagua Config kisha chagua default alafu bofya mara moja kwenye file ambalo limeandikwa common.php kisha chagua Edit kwenye menu itakayo tokea.

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Baada ya hapo utaona file lenye code limefunguka, kumbuka unaweza kuona limechelewa kidogo kuonekana ni kitu cha kawaida usishangae sana subiri kidogo na file hilo litaenda kuonekana moja kwa moja.

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Baada ya ufungua file hilo, kwenye ukurasa huu kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu box la kwanza kutoka juu kwenye namba 4 utabadilisha maneno ‘jina la website’ na kuweka jina halisi la website yako.

Box la pili kutoka juu kwenye namba 5 utabadilisha maneno ‘msemo wa website’ na kuandika maelezo mafupi ya website yako, hakikisha maelezo hayo yanakuwa mafupi chini ya maneno 20. pia hakikisha alama za koma zinabakia hata baada ya wewe kuandika jina na msemo wa website yako.

Hatua ya mwisho, kwenye box la tatu kutoka juu kwenye namba 9 badilisha maneno ‘tovuti ya muziki angalia tanzania tech kujua jinsi ya kutengeneza’ na andika maelezo marefu kuhusu website yako, hii ni muhimu kwani maelezo haya yataonekana kwenye Google pala mtu atakapo tafuta jina la tovuti yako.

Hakikisha pia alama za koma zinabaki kama zilivyo hata baada ya kufanya mabadiliko hayo.

Baada ya hap malizi kwa kubofya kitufe cha kusava kilichopo chini upande wa kulia na baada ya hapo moja kwa moja unaweza kuona tovuti yako imebadilika jina pamoja na msemo wake.

Kuweka Matangazo

Basi baada ya kufuata hatua hizi sasa ni sehemu ya mwisho ambayo ni sehemu ya kuweka matangazo, unacho takiwa kujua ni kuwa Google Adsense haipokei tovuti za kudownload nyimbo hivyo ni muhimu kuomba matangazo kwenye tovuti nyingine zinazotoa huduma sawa na Google.

Tovuti moja wapo ambayo ni bora kwa sasa yenye kutoa kiwango nafuu cha pesa ni tovuti inayoitwa Propush, hii ni website ambayo inakuja na matangazo ambayo yanakuja kama sehemu ile ya kupewa habari mpya kwenye tovuti yaani push notification.

Kupitia tovuti hiyo utalipwa kwa kila mtu atakaye weza kujisajili na notification yako kupitia tovuti yako, sasa ili kujisajili fuata njia hizi.

Tembelea tovuti ya Propush.me hapa, baada ya hapo bofya bendera ya uingereza iliyopo juu upande wa kulia, baada ya hapo bofya kitufe cha Register kitakacho tokea kati kati ya kioo chako.

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Baada ya kubofya Register utaletwa kwenye fomu ambayo unatakiwa kujaza kwa umakini kwani kuna baadh ya vitu hutoweza kubadilisha baadae. Baada ya kukamilisha usajili utatumiwa barua pepe yenye link ya kuhakiki usajili wako hivyo bofya Verify Account kuhakiki usajili wako.

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Baada ya hapo sasa ingia kwa kutumia password au nywila na barua pepe yako ambayo ulijisaili nayo awali kisha moja kwa moja bofya sehemu ya Add Source. Bofya hapo kisha chagua Website alafu andika jina la website yako kisha maliza kwa kubofya Add site.

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakawa kupakua file kwa ajili ya kuweka kwenye domain yako, bofya kitufe cha download kwa ajili ya kupakua file za html kisha moja kwa moja nenda kwenye website yako kwenye sehemu ya file manager kisha fungua hadi kwenye ukurasa ule wa htdocs kama inavyo onekana hapo chini.

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Baada ya kufungua file hilo la htdocs moja kwa moja ndani ya file hilo bofya sehemu ya chini yenye mshale unao angalia juu kisha chagua Upload File.

Chagua mahali ulipo download file lile la html, file hilo mara nyingi linakuwa halina jina bali ni namba namba pamoja na herufi chagua kisha upload.

Tengeneza Tovuti ya Muziki Kwa Kutumia Smartphone (Bure)

Baada ya kuweza ku-uploda kikamilifu basi moja kwa moja rudi kwenye ukurasa ule wa propush kisha bofya kitufe cha Verify, kama itakuwa imekataa, subiri kwa muda kidogo propush waweze kupitia tovuti yako kisha rudia tena kubofya Verify.

Ukisha kubaliwa sasa endelea kwenye hatua ya mwisho ya kutengeneza code za matangazo, hapo unatakiwa kubofya sehemu ya Create smart Tag, kisha baada ya hapo changua Rev. share alafu bofya Create.

Baada ya hapo utaletewa ukurasa ambao unatakiwa kupakua file, bofya sehemu ya Download kisha nenda kwenye file like la htdocs ndani yake alafu upload file kisha chagua file hilo, baada ya hapo rudi tena kwenye website kisha bofya verify. Baada ya hapo kama haito fanikiwa mara moja subiri kidogo kisha jaribu tena.

Baada ya hapo moja kwa moja utakuwa uko tayari kuanza kupata pesa kupitia tovuti yako mpya ya muziki. Unaweza kuona tovuti hii inalipa kiasi cha dollar 11 kwa subscriber utakao wapata, ikiwa kiwango hicho kinaweza kubadilika kutokana na mfumo yaani windows au simu pamoja na siku husika.

Doooh… hadi hapo tutakuwa tumefikia mwisho wa njia ya kutengeneza tovuti hii pamoja na kupata pesa, kama kuna mahali utakuwa umekwama basi usisite kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Kwa Msaada Zaidi Guys Uliza Swali Kupitia Hapa itakuwa ni Rahisi Kusaidia Kila Mtu

Pia kama unataka kusaidiwa kufanya hatua hizi unaweza kuwasiliana nasi kwa kutumia fomu inayo patikana kwenye ukurasa huu. Mpaka siku nyingine guys endelea kutembelea Tanzania Tech.

22 comments
  1. Mkuu mbona nikitaka kuedit hilo file kwenye hatua ya 3 na ya mwisho inagoma? kwa mfan nikitak kuedit “jina la website”haikubali kwanin?

        1. Apo juu nilishindwa kukamilisha hatua ya 3 jinsi ya kuedit lile file la muziki yaani nimemaliza vipengele vyote ila kwenye kuyafuta yale maneno mfano “jina la website”ili niandike langu inashindikana kabisa mkuu

          1. Pole sana unaweza kuuliza swali lako kupitia forum yetu tutakusaidia kwa ukaribu zaidi.

  2. Mkuu najaribu kutumia forum lakin inasumbua imegoma kusend wala kureply text yoyote japokuwa nishajiunga na kuactivate forum email

          1. Nimeshindwa kubadilisha jina la website,msemo wa website na taarifa kuhusu website.kiufupi kwenye kuedit lile file letu la mziki

  3. shida yangu ni pale kwenye kufuta neno kwa mfano “jina la website” nikitaka kulidelete ili niandike langu inagoma kufanya ivyo je nifanyaje mkuu

  4. nimeshindwa kufuta maneno kama “jina la website”msemo wa website” ili niandike yangu kwani kila nikijaribu kuyafuta haiwezekan yanabak ivyoivyo nifanyaje?

  5. Nimekujibu kuwa simu yangu imegoma kuwa accessed na hiyo forum ya kuuliza maswal thus why nikaomba unisaidie ila naona Wali???

  6. nitumie namba yako ya WhatsApp kunasehe mu inanishinda sheheya ya kwanza hatua ya mwisho ile nyimbo azitokei

  7. Ndg hongera kwa kazi nzuri ,,elimu unayotoa ,, Ni nzuri ,,najifunza kupitia makala zako ,, maelezo yanaeleweka

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use