Hivi karibuni masoko ya mtandaoni yamekuwa na umuhimu mkubwa sana hasa kipindi hichi ambapo virusi vya corona vimelazimisha watu kukaa nyumbani na kutumia mtandao zaidi.
Kuliona hili hivi leo nimekuletea makala ambayo nitakujulisha njia rahisi za kuweza kuanzisha soko lako la mtandaoni ikiwa pamoja na kumiliki soko hilo kwa asilimia 100. Kumbuka njia hizi ni za bure kwa asilimia 100 hivyo huna haja ya kulipia kitu chochote zaidi ya kuchagua njia moja utakayo ipenda na kuinstall mfumo huo kwenye domain na hosting yako.
TABLE OF CONTENTS
X-Cart
Mfumo wa X-Cart ni mfumo wa bure kabisa ambao unaweza kukusaidia kuanzisha soko la mtandaoni kwa haraka. Mfumo wa unaweza kuinstall kwenye hosting yoyote na unaweza kuuza bidhaa zako mtandaoni mara baada ya kumaliza kuinstall mfumo huu. Unaweza kuangalia mfumo wa tovuti hii kwa kubofya sehemu hapo chini au bofya Download kupakua mfumo huu.
PrestaShop
PrestaShop ni mfumo mwingine ambao unaweza kutumia kuanzisha soko lako la mtandaoni, kama ilivyo X-Cart, mfumo huu pia ni wabure kwa asilimia 100 na unaweza kupakua mfumo huu na kuinstall na kuanza kutumia kuuza bidhaa kwa haraka. Uzuri wa mfumo huu unakuja na addod za PesaPal ambazo zinaweza kukusaidia kupokea malipo kwa kutumia Mobile Money (M-Pesa, Tigo Pesa na mitandao mingine). Unaweza kuangalia mfumo wa PrestaShop hapo chini.
Bagisto
Bagisto ni mfumo mpya na wabure ambao unaweza kukusaidia kuanzisha soko la mtandaoni lenye muonekano bora sana. Kama unatafuta njia bora na ya kisasa ya kuuza bidhaa zako basi jaribu mfumo huu wa Bagisto. Tatizo la mfumo huu ni ngumu kwa mtu asiye na ujuzi ku-install mfumo huu, unaweza kuangalia mfano wa mfumo huu hapo chini.
WooCommerce
WooCommerce ni sehemu ya mtandao wa wordpress, kupitia mfumo huu unaweza kufanya yote yanayo fanywa na mifumo yote hapo juu, unaweza kutengeneza soko la kisasa, unaweza kupata njia za kupokea pesa kupitia mitandao ya simu na mambo mengine mengi. Mbali ya yote mfumo huu unakuruhusu kuweza kuunganisha mfumo huu na programu za Android na iOS.
Open Cart
Open Cart ni mfumo mwingine wa bure ambao ni wa bure kabisa ambao pia unaweza kukusaidia kuanzisha soko la mtandaoni, mfumo huu pia inakuja na uwezo bora wa kukusaidia kuanzisha soko la kisasa lenye uwezo bora na muonekano mzuri. Pia vile vile unaweza kutumia plugins au addon za kuongeza uwezo wa mfumo huo ikiwa pamoja na kuwezesha njia za malipo ya simu kama M-Pesa na Tigo Pesa.
Magento
Magento ni mfumo mwigine ambao unaweza sana kukusaidia kuanzisha soko la mtandaoni, mfumo huu pia unaweza kuongezewa uwezo kwa kutumia plugin na addon na kufanya mfumo huu kuwa bora sana. Mfumo huu unatumiwa na kampuni kubwa kama vile cocacola na kampuni nyingine kubwa, mfumo huu pia unahitaji kuwa mtaalam kidogo ili kuweza kuendesha na kutumia kikamilifu.
Na hiyo ndio baadhi ya mifumo ambayo inaweza kukusaidia sana kuanzisha soko lako la mtandaoni, kama unataka kuanzisha mfumo moja ya mfumo kwenye list hii unaweza kupakua mfumo huo na kuinstall kwenye hosting yako kwa haraka na urahisi.
Kama unahitaji msaada zaidi au kuna mahali popote umekwama unaweza kuwasiliana nasi kupitia sehemu ya maoni hapo chini, mpaka siku nyingine endelea kutembelea Tanzania Tech.