Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Njia Mbili Mpya za Kutengeneza Pesa Mtandaoni (Tanzania)

Utaweza kupata pesa mtandaoni hapa Tanzania
tengeneza pesa mtandaoni tengeneza pesa mtandaoni

Kutengeneza Pesa mtandaoni ni moja kati ya kazi inayo tafutwa na watu wengi sana hasa hapa Tanzania, lakini kwa sababu teknolojia inatumika kwa kiwango kidogo hapa Tanzania, njia za kutengeneza pesa mtandaoni hasa kwa hapa Tanzania zimekuwa ngumu sana na hadimu.

Lakini leo hapa Tanzania Tech tumefanikiwa kupata njia mbili ambazo zinaweza kusaidia kupatia pesa mtandaoni kama utakuwa unafanya kazi hizi kwa bidii na kwa kuzingatia. Njia hizi zinafanya kazi asilimia mia moja na watu wengi wanaendesha maisha yao kupitia njia hizi. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia hizi.

Advertisement

  • Weka Video Zako Kwenye Mtandao wa Rumble.

Tofauti na mitandao mingine kama YouTube, mtandao wa Rumble wenyewe unalipa watumiaji wake kwa umaarufu wa video. Endapo unaweza kutengeneza video inayoweza kuangaliwa na watu wengi dunia nzima basi unaweza kutengeneza kiwango kikubwa sana cha pesa kupitia mtandaoni. Mbali na hayo mtandao huu unaweza kusambaza video zako kwenye mitandao mikubwa kama CNN, Yahoo na mitandao mingine yenye kuonyesha Video na hivyo itakufanya uweze kupata pesa zaidi na zaidi. Kitu cha muhimu ni kuhakikisha video yako inakuwa maarufu na ina angaliwa na watu wengi zaidi.

Kama wewe unajua unaweza kutengeneza video maarufu, unaweza kujiunga na mtandao wa Rumble Hapa, vilevile unaweza kujua zaidi kuhusu mtandao huo kwa kusoma zaidi hapa. Unaweza kuona hapa chini picha mtandao wa rumble video zikiwa zimeingiza pesa nyingi kwa idadi ya Views.

  • Fungua Akaunti ya Supporter Kupitia Tovuti ya BeForward

Kama wengi wenu mnavyojua befoward ni moja kati ya kampuni kubwa zinazofanya biashara za magari hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, mbali na kufanya biashara ya magari hivi karibuni kampuni hiyo imeanza kuuza bidhaa za kieletroniki kupitia mtandao wake wa beforward. Mbali na huduma zote hizo, mtandao wa befoward pia unakuja na njia ya kujipatia pesa mtandaoni kupitia njia za kuuza magari na vifaa vingine vya kielektroniki.

Unachotakiwa kufanya ni kujisajili na akaunti ya beforward supporters kisha utapata namba maalum ambayo pale mtu atakapo nunua gari au vifaa vya kieletroniki kupitia mtandao huo na kuweka namba yako, basi aliye nunua gari ataweza kupata punguzo la bei na wewe pia utapata pointi ambazo baadae unaweza kubadilisha pointi hizo kuwa pesa taslim. Mbali na hayo kama ukifanikiwa kuuza bidhaa nyingi utaweza kuingia kwenye tuzo maalum za kila mwezi na utapata zawadi.

Unaweza kujiunga na beforward supporters Kupitia Hapa, pia unaweza kusoma zaidi kuhusu beforward supporters Hapa. Unaweza kuona hapo chini baadhi ya watu kutoka nchi mbalimbali walivyo jipatia pesa kupitia njia hii.

Na hizo ndio njia mbili ambazo nimekuandalia kwa siku ya leo, Njia hizi ni baadhi ya njia ambazo tumefanya uchunguzi na kujua kweli zinalipa kwa asilimia 100. Ili kujua njia nyingine zilizobaki pale tutakapo maliza kufanya uchunguzi, hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech, au hakikisha unapakua app ya Tanzania Tech kupata maujanja zaidi ya njia zilizo baki.

Kama unataka kujua njia nyingine za kujipatia pesa mtandaoni kupitia simu yako ya mkononi, unaweza kusoma hapa pia kama unataka kufanya biashara mtandaoni na kupata pesa unaweza kusoma hapa.

7 comments
  1. Mwandishi nakupa pongezi kwa App yako ya Tanzania Tech. Kwa kweli kuna mambo muhimu nilikuwa nahitaji kufahamu kwa undani zaidi ila muda wangu ni finyu sana.

    Moja ya mambo ni kama haya uliyozungumzia kupitia mada hii. Naomba nikupongeze kwa kazi nzuri unazozifanya. Kwa kweli mimi nitakuwa na app yako bega kwa bega kutokana na ukweli kuwa mambo ya tech nafuatilia sana na ndio interest yangu kubwa.

    Nina imani nitajifunza mambo mengi kwako na tuta share ideas kuendelea kupanua Elimu katika uwanja wa Tekinolojia.

    Asante

  2. Naomba kuuliza kabla sijajiunga,je kuna gharama yoyote ya kujiunga kuwa supporter? Pia nikijiunga napewa mwongozo wa jinsi ya kufanya kazi?

  3. Hongera sana Tanzania Tech,nimewaelewa vizuri, lakini nimewatumia Email mara kadhaa sipati majibu

    1. Email zinajibiwa mbona, inawezekana haijatufikia. Tafadha tumia fomu inayopatika kwenye sehemu ya wasiliana nasi.

  4. Maoni*mwandishi mm naomba muongozo kamili wakujiunga na be forward sababu nimejaribu but nimeshindwa

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use