Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Template ya Blogger inayoweza Kusaidia Kupata Pesa Mtandaoni

Tengeneza blog ya kuruhusu kudownload android apps mbalimbali
Template ya Blogger inayoweza Kusaidia Kupata Pesa Mtandaoni Template ya Blogger inayoweza Kusaidia Kupata Pesa Mtandaoni

Mwaka 2020 tayari umeanza na leo ni siku ya 11 kati ya siku 30 za mwezi huu wa kwanza, Kwa kusema hivi najua wengi wenu tayari mnayo malengo ya kibiashara kwenye mwaka huu hasa wale ambao wanafikiria kufanya biashara za mtandaoni.

Kupitia mwaka huu 2020 Tanzania Tech tunaahidi kukuletea makala nyingi zaidi ambazo zitakusaidia kuweza kutengeneza biashara yako mtandaoni ikiwa pamoja na njia za kuweza kupata pesa kupitia mtandaoni.

Advertisement

Lakini kabla ya yote labda tuanzie hapa leo, kupitia makala hii ya leo nime kuandalia template ya blogger ambayo inaweza kukusaidia kupata pesa kwa urahisi mtandaoni. Uzuri wa template hii ni kuwa unaweza kuipata bure kabisa bila kulipia hata shilingi kumi, na kwa kufanya hivyo moja kwa moja utaweza kuanza biashara yako mtandaoni bila kulipia kwani wote tunajua blogger ni mtandao wa bure. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie templent hii.

Template ya Blogger inayoweza Kusaidia Kupata Pesa Mtandaoni

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao kwa namna moja ama nyingine unataka kuanza kutengeneza kipato mtandaoni kwa haraka kwa kutumia blogger basi templent ya Pure APK ni bora sana kwako. Uzuri wa templent hii ni kuwa ina sehemu nyingi za matangazo na pia utaweza kutengeneza pesa kwa haraka kupitia Adsense.

Kitu ambacho ujajua kuhusu Adsense ni kuwa, kama unayo website ambayo ina ruhusu download ambazo ni halali basi una uhakika wa kuingiza pesa zaidi kuliko mtu mwenye website kwa mfano kama hii ya Tanzania Tech. Hii ni kwa sababu katika list ya topic au mada za website ambazo zinaingiza pesa nyingi zaidi kupitia Adsense basi Downloads ni topic ya kwanza.

Hii ni kwa sababu Adsense ina hitaji zaidi tovuti ambayo watumiaji watabonyeza matangazo yaliyopo kwenye website, yaani ni sawa na kusema kuwa, mtumiaji wa tovuti ya download ana tegemewa kubonyeza au ku-click mara nyingi zaidi kwenye website hiyo kuliko mtumiaji wa tovuti ya habari kwani huyo hubonyeza mara moja ama mbili hadi kupata anachokitaka, Soma zaidi hapa.

Template ya Blogger inayoweza Kusaidia Kupata Pesa Mtandaoni

Jinsi ya Kutumia Template Hii

Sasa ili kusudi uweze kupata pesa kwa kutumia template hii ya Pure APK basi ni muhimu kujua jinsi ya kutumia, hapa sizungmzi jinsi ya kuweka template kwenye blogger bali ni jinsi gani unaweza kutumia tamplate hii kuweza kukubaliwa kwenye Adsense.

Kama ulivyoweza kuona kwenye picha hapo juu template hii ni kwajili ya apps za android na unaweza kuchagua apps ambazo ungependa kuruhusu watu kupakua, unaweza kuamua kuweka apps za kitanzania pekee au ukaweka apps za kundi lolote lile lakini hakikisha usifanye mambo haya.

  • Usiweka apps za Cracked kwani hutopewa matangazo
  • Usiandike Blog yako kwa kiswahili
  • Usiweke apps zinazo julikana sana kama vile Instagram, Facebook na nyingine kama hizo kwani hizi watu wanazijua na hutopata watu wakupakua.
  • Kama unatumia website nyingine kama apk mirror kunakili app hakikisha una nakili kwa kutumia akili na usinakili kama ilivyo.
  • Hakikisha huweki file lolote kwenye kwenye website yako, weka link tu ambazo zitakuwa zinawapekeka watumiaji kwenye website nyingine kwaajili ya kupakua apk. Unaweza kutumia tovuti ya link kama hii hapa ili kuongeza kipato.
  • Usiombe matangazo haraka, fanyia kazi website yako kwa muda wa wiki mbili hadi mwezi ndio uombe matangazo, Unaweza kusoma hapa kujua hatua za kufanya ili kupewa matangazo.

Baada ya kusema hayo sasa utakuwa upo tayari kuanza safari yako ya kutengeneza pesa kupitia mtandao kwa mwaka huu 2020. Unaweza kuangalia mfano wa template hiyo ikiwa kwenye kwenye website kupitia hapo chini pia unaweza kupakua Template hiyo kupitia hapo chini

Demo Hapa

Download Hapa

Kama utakuwa umekwama mahali popote unaweza ku-uliza swali lako kupitia sehemu ya maoni hapo chini, kujifunza zaidi jinsi ya kupata pesa mtandaoni hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kwani tutakuletea makala nyingine nzuri zaidi ambazo zitakusaidia kutengeneza pesa mtandao kwa haraki.

7 comments
  1. naomben kujuwa jins ya kutafuta simu iliyo potea kwa kutumia imei za simu

    how to find my slost phone by using imei nomber

  2. Nahitaji usaidizi wako maana mi nimejalibu kuweka templet kwenye blog yangu ‘nimeshidwa naomba unisaidie kuweka templet kwenye blog yangu

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use