Kama wewe ni mmoja wa watengenezaji wa maudhui mtandaoni basi habari njema kwako kwani hivi karibuni mtandao wa YouTube unategemea kuanza kulipa watengenezaji wa video za dakika 1 maarufu kama YouTube Shorts.
Habari hizi zinakuja hivi karibuni huku kukiwa na mabadiliko machache ambayo pengine yanaweza kusaidia watengenezaji wa maudhui ya video kutengeneza kipato kwa urahisi zaidi kupitia mtandao wa YouTube.
Hadi sasa kwa hapa Tanzania mtandao wa TikTok ambao ndio mtandao unaongoza kwa video za wima, bado hauja anza kulipa watengenezaji wa video hizo.
Hii inatoa nafasi wa watengenezaji wa video hizo kurudi kwenye mtandao wa YouTube kwenye kipengele cha video za wima (Shorts) kwani hivi karibuni watumiaji wote hapa Tanzania wataanza kulipwa kutokana na video hizo.
TABLE OF CONTENTS
Jinsi ya Kulipwa Kupitia Video za YouTube Shorts
Kwa mujibu wa YouTube, kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2023 utaweza kuanza kutengeneza pesa kupitia mtandao wa YouTube kwa kuomba matangazo ya YouTube kupitia video za kawaida na pia video za YouTube Shorts.
Kwa mujibu wa taarifa hii mpya, watengenezaji wa maudhui ya video kupitia mtandao wa YouTube wanaweza kujiunga kwenye YouTube Partner Program au YPP kwa kuwa na Subscribers 1000 pamoja na 4000 watch hours ndani ya miezi 12, au Subscribers 1000 na watch hours milioni 10 kupitia video za YouTube Shorts ndani ya siku 90.
Mbali na hayo pia YouTube itakuja na njia mpya ya Mgawanyo wa mapato kwa watengenezaji wa Video za YouTube Shorts na kusaidia watengenezaji kubakiwa na hadi asilimia 45% za mapato yote baada ya mgawanyo huo. Kumbuka mapato hayo yanategemeana na idadi ya views.
Wasanii Kutengeneza Pesa Kupitia YouTube Shorts
Mbali na YouTube kutangaza njia ya kutengeneza pesa kupitia YouTube Shorts kwa watu wote, hivi karibuni wasanii wataweza kutengeneza pesa kupitia sehemu mpya ambayo itawasaidia kujitangaza zaidi na kupata pesa zaidi.
YouTube imetangaza kuja na sehemu mpya ya Creators Music, sehemu hii itasaidia wasanii kuweza kuuza nyimbo zao kwa mfumo wa leseni na kuruhusu watengenezaji wa video kununua leseni hizo kwa ajili ya kutumia nyimbo kwenye video zao ndani ya mtandao wa YouTube.
Kwa kununua leseni ya nyimbo kutoka kwa msanii utaweza kutumia nyimbo husika kwenye mtandao wa YouTube huku ukitengeneza pesa kwa matangazo bila kupata tatizo la Copyright Claim.
Pia wasanii wataweza kukuza nyimbo zako kupitia sehemu ya Creators Music kwa mfumo au leseni ya kugawana mapato ambapo watengenezaji wa video wataweza kuchagua kutumia muziki bila kulipia na kugawana mapato na wamiliki wa nyimbo au muziki ulio tumika. Mtumiaji anaweza kuchagua kati ya leseni hizo mbili kupitia sehemu ya Creators Music.
Mabadiliko Mengine
Mabadiliko mengine ambayo yanakuja kwenye mtandao wa YouTube ni pamoja na watumiaji wa mtandao wa YouTube waliopo kwenye YPP au YouTube Partner Program wanatakiwa kusign makubaliano mapya ambayo yatakuwa yanaelekeza zaidi njia mpya ya kutengeneza pesa kupitia YouTube Shorts hivyo kila mwenye channel yenye uwezo wa kuonyesha matangazo anatakiwa kusign makubaliano hayo kwa kukubali vigezo na masharti mapya ya YPP.
Maelezo zaidi jinsi ya kusign vigezo hivyo vipya yatatumwa kupitia barua pepe kwa watumiaji wote wa YouTube YPP ifikapo mwanzo wa mwaka 2023.
Na hayo ndio baadhi ya mabadiliko ambayo utegemee kuyaona kupitia YouTube Shorts pamoja na YouTube kwa ujumla. Kumbuka kama sasa huja anza kutengeneza video za Shorts ni wakati wa kufanya hivyo kwani utaweza kutengeneza pesa kwa urahisi kupitia YouTube Shorts.
Kama unataka maelezo zaidi ya mabadiliko hayo unaweza kuangalia video hapo juu, au unaweza kutembelea tovuti ya YouTube hapa.
Nawezaje kutengeneza pesa mtandaoni
Endelea kutembelea Tanzania Tech
Ni program ipi inayolipa moja kwa moja kwa namba ya simu?