Kama wewe ni mtumiaji wa muda mrefu wa mtandao wa instagram ni wazi kuwa umeshawahi kuona picha za instagram za Grid na panorama crop, picha hizi kuwa kwenye mitindo mbalimbali ambayo huvutia sana hasa pale inapotumika kutoa ujumbe fulani.
Kama unavyoweza kuona picha hapo juu, huo ni mfano wa kwanza wa Grid panorama crop, ambapo picha moja inaweza kugawanyishwa na kuwa picha tisa au zaidi ili kuunganisha picha moja pale mtu anapo angalia post zako kwa ujumla kupitia kitufe cha Instagram grid.
Aina nyingine ya panorama crop ni pamoja na Swipeable Panorama ambayo huweza kugawa picha moja ambayo ina urefu kwa upana na picha hiyo kuwekwa kwenye vipande vitatu au zaidi kwenye post za “swipe left” kupitia mtandao wa instagram. Pale mtu anapo slide kwenda kushoto huweza kuona muendelezo wa picha husika kama unavyoweza kuona hapo juu.
Jinsi ya Kutengeneza Swipeable Panorama
Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kutengeneza post kama hizo hapo juu basi unaweza kufanya hivyo kwa kufuata hatua hizi chache.
Kwa kuanza pakua app ya Panorama Crop for Instagram, unaweza kupata app hii kupitia play store au unaweza kupakua kupitia link hapo chini.
Baada ya kudownload app hiyo moja kwa moja chagua aina ya Panorama Crop unayohitaji ambayo ni option ya kwanza juu, kisha moja kwa moja chagua picha kutoka kwenye simu yako.
Baada ya hapo unaweza kuchagua unataka kukata vipande vingapi picha hiyo, unaweza kuchagua kukata hadi vipande 10 kwenye picha moja.
Kama unavyoweza kuona hapo juu, picha hii imechaguliwa kukatwa vipande vitatu ambavyo kwa pamoja vinatengneza Swipeable Panorama post bora.
Jinsi ya Kutengeneza Grid Post
Kama nilivyo kwambia kuna aina mbili ambazo zina trend kwa sasa na hizo ni Swipeable Panorama Crop na Grid Crop. Na sasa twende tukangalie jinsi ya kutengeneza Grid Grop.
Kwa kuanza pakua app ya Grid Maker for Instagram, unaweza kupakua app hiyo kupitia hapa au kupitia link hapo chini.
Baada ya ku-downlad app hii moja kwa moja fungua app hii kisha chagua picha na kisha endelea kwa kufuata maelekezo hapo chini.
Bila shaka kwa kufuata hatua hizo hapo juu utakuwa umeweza kutengeneza Grid Crop na Panorama Crop post za Instagram.
Kama kuna mahali utakuwa umekwama unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku, pia unaweza kujifunza zaidi kwa kusoma hapa jinsi ya kuweka font tofauti kwenye post zako za Instagram.