Kwa mfanya biashara yoyote ni muhimu kuwepo kwenye mitandao ya kijamii, lakini mbali ya mitandao ya kijamii zipo sehemu nyingine mbalimbali ambazo ni muhimu sana biashara yako kuonekana.
Google My Business ni moja ya sehemu ambayo kila mfanya biashara anatakiwa kuweka biashara yake, hii ni muhimu sana hasa kama bishara yako inayo eneo maalum la biashara (Business Location).
Kuptia Google My Business unaweza kupata faida nyingi sana kama kuonekana kupitia Google hivyo kupatikana na wateja wako kirahisi hasa pale wanapo kutafuta kupitia Google Search.
Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia kuweza kuweka biashara yako moja kwa moja kupitia Google My Business. Hatua hizi ni rahisi na haraka hakikisha unafuatilia makala hii mwanzo hadi mwisho. Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi twende kwenye makala hii.
TABLE OF CONTENTS
Kutengeneza Ukurasa wa Google My Business
Kama unavyoweza kuona hapo juu, huo ni mfano wa ukurasa wa Google My Business wa Tanzania Tech Media, unaweza kupata ukurasa kama huo kwa kufuata hatua zote zifuatazo.
Mahitaji ya Muhimu
Kabla ya kuanza ni vyema kuwa na mahitaji yafuatayo, mahitaji haya yataweza kusaidia kukamilisha usajili wako haraka zaidi.
- Namba ya Simu ya Biashara
- Sanduku la Posta
- Akaunti ya Google (Gmail)
- Anwani ya Mahali Biashara yako Ilipo
- Maelezo ya Muhimu ya Biashara yako
Kama tayari unayo mambo yote hayo basi moja kwa moja unaweza kuendelea kwenye hatua za kutengeneza Google My Business kwa ajili ya biashara yako.
Hatua za Kufanya
Hatua ya kwanza unatakiwa kutembelea tovuti ya Google My Business, unaweza kupata link kupitia hapo chini.
Baada ya kutembelea ukurasa huo unatakiwa kubofya sehemu ya Sign in, sehemu hii inapatikana juu upande wa kulia kama unatumia kompyuta, na kama unatumia simu inapatikana kwenye Menu iliyopo kushoto, baada ya kufungua menu hiyo angalia mwisho kabisa.
Baada ya hapo, unatakiwa kuingia kwenye akaunti yako ya Google (Gmail), baada ya kuingia utapelekwa kwenye uwanja ambapo unatakiwa kuandika jina la biashara yako.
Andika jina la biashara yako kwa usahihi kisha bofya chini linapo tokea jina hilo baada ya kumaliza kuandika. Baada ya hapo unatakiwa kuweka Category ya biashara yako, sehemu hii ni muhimu kwa kuonyesha biashara yako ni ya aina gani.
Wakati una andika Category utaweza kuona mapendekezo mbalimbali kulingana na neno ulilo andika, chagua pendekezo linalo fanana na aina ya biashara uliyo changua.
Baada ya kumaliza kuchagua kipengele au Category, moja kwa moja bofya kitufe cha next kilichopo chini ya maelezo hayo.
Baada ya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa mwingine ambapo sasa unatakiwa kuchagua kama unataka kujaza sehemu ya location au eneo ambapo biashara yako inapatikana, kama unalo eneo chagua Yes, kama huna eneo changua No.
Google My Business inafaa zaidi kama unalo eneo, kwani hii itakusaidia kuweza kuonekana kwenye Google Maps. Hii haina maana kuwa huwezi kutengeneza ukurasa huu kama huna eneo la biashara.
Ni muhimu kufahamu kuwa maelezo ya kuendelea kuanzia hapa yana tofautiana kulikanga na majibu ya swali hilo la kama una eneo la biashara au huna eneo la biashara. Kwa sasa tuangalie kama mtu unalo eneo la biashara.
Baada ya kuchagua Yes, moja kwa moja utapelekwa kwenye fomu hapo juu, unatakiwa kujaza mahali ambapo biashara yako inapatikana. Kwenye sehemu ya Street Andress, andika mahali biashara ilipo kwa mfano unaweza kuandika Kinondoni, Studio House Number 8.
Kwenye sehemu ya Postal Code andika sanduku la posta, hii ni muhimu sana kwani sanduku hilo litatumika kuhakiki biashara yako ilipo hivyo kuwa makini na hili.
Sehemu ya mwisho ya City, andika mkoa ambapo biashara yako inapatikana, kama unapatikana Moshi basi andika Moshi, au kama ni Dar es salaam pia andika hivyo hivyo.
Hii inafanya anwani yako kwa ujumla kuwa kama hivi, Mfano hapo juu utakuwa Kinondoni, Studio, House Number 8, Dar es Salaam, Tanzania.
Baada ya kujaza data hizo, moja kwa moja bofya Next kisha utapelekwa kwenye ukurasa wenye ramani ambapo unatakiwa kuchagua mahali ambapo biashara yako inapatikana. Google itachagua ramani yenyewe kulingana na anwani au adress uliyo chagua kwenye hatua iliyopita.
Hakikisha biashara yako ipo kwenye eneo lililo chaguliwa au unaweza kutauta endeo ambalo upo kwa muda huo kwa kuruhusu sehemu hiyo ya ramani kujua mahali ulipo.
Baada ya hapo malizia kwa kubofya Next, hatua inayo fuata utaulizwa kama unatoa huduma za wateja kuja ofisini au unafanya delivery ya huduma. Kama jibu ni ndio chagua Yes kama ni hapana chagua No.
Hatua ya Muhimu
Hatua ya muhimu ni kuweka namba yako ya simu pamoja na tovuti, hii ni muhimu sasa kwani Google sasa hutumia njia ya simu kama njia kuu ya kuweza kuthibitisha ukurasa wako wa Google My Business. Hivyo ni vizuri kuandika namba ya simu ya biashara yako pamoja na tovuti.
Hatua inayo fuata utaulizwa maeneo ambayo unatoa huduma, sehemu hii unatakiwa kujaza maeneo ya karibu na eneo ulilopo au kama unatoa huduma kwa nchi nzima basi andika Tanzania kabisa kisha bofya next. Kumbuka unaweza kuchagua eneo zaidi ya moja.
Kumbuka hatua hiyo pia sio ya lazima unaweza kuachana nayo na kuendelea na hatua nyingine.
Baada ya hapo bofya Next kisha utapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakiwa kuja mawasiliano yako. Unatakiwa kujaza Namba ya simu ambayo utatumia kupigiwa na wateja, utajaza website kama unayo na pia kama huna utaweza kutenegeneza website ya bure hapo hapo.
Baada ya hapo moja kwa moja utamalizia kwa kubofya Next, kisha utabofya Yes, na moja kwa moja utapelekwa kwenye hatua ya mwisho ya kuthibitisha biashara yako.
Baada ya hapo chagua siku ambazo biashara yako ipo wazi, kama hutaki kujaza hili kwa sasa bofya Skip. Pia utaletewa sehemu ya kuweka maelezo kuhusu biashara yako na hapa pia kama hutaki kujaza kwa muda huo utabofya Skip.
Baada ya hapo fuata maelekezo hadi mwisho na utaweza kupata ukurasa wako wa Google My Business. Kama unataka kupata ukurasa wako kwa haraka hakikisha unaweka anwani ambayo inapatikana ndipo utakuwa tayari kwa haraka kupata ukurasa wako bila kufanya uthibitsho wowote.
Hitimisho
Najua kuwa maelezo ni mengi kidogo, hivyo kama kuna mahali popote ambapo utakuwa umekwama basi usisite kuwasiliana nasi au unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kitu cha muhimu ni kuwa ukitaka kuendesha biashara yako kupitia Google sasa unatakiwa kutafuta jina la biashara yako na moja kwa moja utaweza kubadilisha au kuongeza chochote kwenye ukurasa wako wa Google Business.
Kwa maujanja zaidi kuhusu biashara mtandaoni nakualika usome makala zetu za jinsi ya kutengeneza pesa mtandaoni, pia hakikisha unasoma maana ya cpc, cpm kupitia google Adsense ili kuanza kutengeneza pesa mtandaoni kupitia Google Adsense.