Kama wewe ni mmoja wa watu ambao bado wanawalipa watu waweza kutengeneza business card pamoja na kadi mbalimbali za mwaliko kwa ajili yako basi makala hii ni yako.
Kupitia makala hii nitakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza kadi za biashara au business card ikiwa pamoja na kadi za mwaliko. Basi bila kuendelea kupoteza muda twende kwenye makala hii.
Kwa kuanza napenda nikwambie kuwa, unaweza kutengeneza kadi hizi zote kupitia simu yako ya mkononi na pia kupitia kompyuta yako. Unaweza kufanya hivyo kwa kupakua app maalum kulingana na mfumo unaotumia Android au iOS.
TABLE OF CONTENTS
Hatua ya Kwanza
Hatua ya kwanza tembelea tovuti ya canva.com, kama unatumia simu za Android au iOS basi unaweza kupakua app husika kupitia link hapa kwa iOS au hapa kwa Android. Pia unaweza kutumia link hapo chini na moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa app husika.
Hatua ya Pili
Baada ya hapo hakikisha unatengeneza akaunti, unaweza kutumia mitandao yako ya kijamii kutengeneza akaunti kwa haraka, hii pia itakusaidia kwani utakuwa huna haja ya kuandika password kila mara unapota kuingia kwenye akaunti yako.
Hatua ya Tatu
Baada ya kufanikiwa kuingia kwenye akaunti yako sasa bofya sehemu ya Templates kisha chagua Cards, Kupitia ukurasa huo utapata mifano mingi sana ya kazi ambazo unaweza ku-edit na kuprint moja kwa moja kweye mfumo wa PDF, PNG au JPG.
Pia ili kurahisha zaidi kama unata kadi za mwaliko basi unaweza kuchagua sehemu ya Templates kisha chagua Cards alafu chagua Invitation.
Unaweza kuchagua kadi yoyote unayohita na ukipenda muonekano wowote kati ya mifano mingi unayo ona na moja kwa moja chagua kwa kubofya kadi husika.
Hatua ya Nne
Baada ya kuchagua kadi moja kwa moja sasa utafunguka ukurasa ambao utakuruhusu kuweza ku-edit kadi yako na kuifanya iwe yako kwa asilimia 100. Kuedit ni rahisi sana kwani unacho takiwa kufanya ni kugusa sehemu unayotaka ku-edit na moja kwa moja utaweza ku-edit.
Kama unataka kuedit maneno unaweza kugusa sehemu za maneno na kisha andika maneno unayotaka mwenyewe, pia kama unata kubadilisha maua na kila kitu kilichopo kwenye kadi hiyo unaweza kufanya hivyo kwa kugusa sehemu husika na kuedit.
Hatua ya Tano
Mara baada ya kubaliza kuediti unaweza kuchapisha au kudownload kadi yako kama pdf ambapo sasa utaweza kupaleka kwaajili ya ku-print. Unaweza kufanya hivyo kwa kubofya Download kisha chagua PDF Print na moja kwa moja utaweza kupata PDF yako kwa urahisi na haraka.
Mfano wa Kadi Niliyo tengeneza
Unaweza kuona mfano hapo chini kadi ya mwaliko niliyo tengeneza kwa njia hii, kama unana kadi hii inaweza kufaa kwa mualiko basi ni wazi njia hii inakufaa kwa asilimia 100. Pia unaweza download mfano huu kwa PDF hapa.
Kutengeneza Business Card
Kwa upande wa kutengeneza Business Card au kadi za biashara basi unaweza kufuta hatua hiza hizo lakini hakikisha unachagua Templates kisha chagua Business Cards. Kupitia ukurasa huo utaweza kuona aina mbalimbali za kadi ambazo unaweza kuedit na kufanya iwe yako kwa asilimia 100.
Uzuri wa kadi hizo zinakuja na pande mbili pande ya nyuma na pande ya mbele ambayo ndio inakuja na mawasiliano ya mtumiaji, upande unao one kwenye picha hapo ni upande wa nyuma.
Hatua za kuedit ni zile zile na utaweza kutengeneza kadi na ku-print card hiyo kwenye mfumo wa PDF au PNG kwa haraka na urahisi. Kizuri ni kuwa utaweza kuprint au kudownload Bussines card yako ikiwa na pande zote mbili.
Mfano wa Business Card Niliyo tengeneza
Na huo ndio mfano mdogo wa kadi niliyo tengeneza kwa kutumia njia hii, unaweza kuendelea kutengeneza kadi yako kwa muundo wowote unaotaka ikiwa pamoja na kuweka logo pamoja na mambo mengine mengi. Pia unaweza kupakua mfano wa PDF hapa.
Na hiyo ndio njia fupi na rahisi ambayo unaweza kutumia kutengeneza kazi za mwaliko au Bussines card kwa urahisi bila kuwa na ujuzi wowote. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unajiunga na channel yetu ya YouTube hapa, pia soma hapa kujua jinsi kufungua app yoyote kupitia sehemu ya Notification.