Kama wewe umekuwa mtumiaji wa App ya Telegram kupitia mfumo wa iOS, basi ni wazi kuwa ni muda mrefu sasa hujaweza kuona au kusasisha toleo jipya la App ya Telegram. Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, kushindwa kusasisha toleo jipya la app hiyo kunakuja baada ya Mamlaka ya Urusi kuamuru Apple kuondoa app ya Telegram kutoka kwenye Soko la App Store mapema mwezi April mwaka huu.
Kwa mujibu wa ujumbe wa Mkurugenzi Mtendaji wa Telegram, Pavel Durov, Apple imekuwa ikizuia app hiyo kusasishwa tokea kipindi hicho hadi sasa, na hiyo ni baada ya mamlaka ya Urusi kuagiza Apple kuondoa App hiyo kwenye soko lake kutokana na kile mkurugenzi huyo alicho sema ni kushindwa kuelewana kati ya kampuni ya telegram na mamlaka hiyo ya Urusi. Hata hivyo App ya telegram imezuiwa kutumika nchini Urusi kuanzia katika ya mwezi wa nne na hiyo ikiwa ni kutokana na sababu hizo hizo ambazo mkurugenzi huyo amezitaja kuwa ni kukataa kutoa programu maalum ya kuruhusu mamlaka ya urusi kuweza kuona data za watumiaji wa App hiyo.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kushindwa kusasisha toleo jipya la App ya Telegram kuna sababisha watumiaji wa App hiyo ambao wanatumia mfumo mpya wa iOS 11.4 kushindwa kutumia baadhi ya sehemu kwenye App hiyo, ikiwa pamoja na kampuni ya Telegram pamoja na App hiyo kwa ujumla kushindwa kufuata vigezo na masharti ya sheria mpya za mtandaoni za GDPR.
Bado hakuna taarifa zaidi kuhusu upande wa App ya Telegram kwa mfumo wa Android, lakini kutokana na sakata ili linavyo endelea uwenda pia app ya Telegram ya Android ikikubwa na sekeseke muda wowote.