Telegram Yaja na Sehemu Mpya ya Kutuma Meseji Bila Sauti

Pia utaweza kuendesha magroup kwa njia bora na yakipekee
Telegram Yaja na Sehemu Mpya ya Kutuma Meseji Bila Sauti Telegram Yaja na Sehemu Mpya ya Kutuma Meseji Bila Sauti

Kama wewe ni mtumiaji wa app ya telegram basi habari njema kwako kwani programu hiyo inazidi kuongezewa sehemu mpya zinazofanya matumizi ya app hiyo kuwa rahisi na bora pengine kuliko programu ya WhatsApp.

Kama ni msomaji wa tanzania tech basi utajua kuwa hivi karibuni telegram iliongeza kipengele cha kuchati na watu mbalimbali walio kuzunguka, sehemu ambayo itakusaidia kuchat na watu usio wajua mtaani au mahali ulipo kwa muda fulani. Lakini kama haitoshi hivi karibuni app ya Telegram imeongezewa sehemu nyingine mpya ambayo inafanya app hiyo kuwa bora zaidi.

Advertisement

Kupitia toleo jipya la app ya Telegram, sasa utaweza kutuma meseji ambazo zikipokelewa kwa uliyemtumia hazitoweza kutoa sauti hata kama mtu huyo simu yake itakuwa imewashwa mlio. Meseji hiyo itaendelea kuonekana kama meseji mpya lakini haito weza kutoa sauti pale inapoingia.

Ili kuwasha sehemu hiyo, unatakiwa kushikilia kitufe cha kutumia (Send) baada ya kuandika meseji yako, kisha utaona sehemu mpya imefunguka ikiwa na maneno “send without sound” bofya hapo na meseji yako itatumwa bila kutoa sauti pale inapofika kwa uliye mtumia.

Telegram Yaja na Sehemu Mpya ya Kutuma Meseji Bila Sauti

Mbali na sehemu hiyo, sehemu nyingine iliyo ongezwa ni “Slow Mode”. Sehemu hii ni kwajili ya viongozi wa magroup (Admin) ambapo kupitia sehemu hii wataweza kuzuia watumiaji kutuma meseji mfululizo.

Telegram Yaja na Sehemu Mpya ya Kutuma Meseji Bila Sauti

Kwa mfano kama unataka mtumiaji fulani asitume meseji mfululizo basi utakuwa na uwezo wa kuzuia mtu asitume meseji kwa hadi meseji moja kila baada ya sekunde 30 mpaka meseji moja kila baada ya lisaa limoja. Kama inavyonekana kwenye picha hapo juu.

Telegram Yaja na Sehemu Mpya ya Kutuma Meseji Bila Sauti

Baada ya kuseti hivyo, mtumiaji ataona sehemu ya saa maalum ikiwa inahesabu muda kwa kupungua, hiyo ikiwa na maana kuwa amezuiliwa kutuma meseji hadi baada ya muda huo kuisha.

Vilevile telegram imeleta sehemu nyingine ya “Admin Titles” sehemu kwaajili ya Admin ambapo sasa admin mkuu ataweza kuweka majina ya ziada mbele ya majina ya Admin wa kawaida ili kuweza kutofautisha admin mmoja na admin mwingine.

Telegram Yaja na Sehemu Mpya ya Kutuma Meseji Bila Sauti

Baada ya kuwasha sehemu hiyo, utaweza kuona jina la ziada likiwa limetokea pembeni ya jina la Admin kila anapotuma meseji, kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Telegram Yaja na Sehemu Mpya ya Kutuma Meseji Bila Sauti

Sehemu hizi zote tayari zinapatikana kwenye app za Telegram za Android pamoja na iOS hivyo kama bado huja sasisha toleo jipya la App hiyo unaweza kufanya hivyo sasa ili kupata sehemu zote hizo. Kama unataka kujua zaidi kuhusu telegram hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use