Hivi karibuni wataalamu wa teknolojia huko marekani wameanza kufanya majaribio ya programu maalaum ya kompyuta yenye uwezo wa kutambua wapenzi wa jinsi moja kwa kuangalia nyuso zao.
Teknolojia hiyo ambayo inafanyiwa majaribio inadaiwa kuwa na uwezo wa kutofautisha watu wapenzi wa kawaida na wapenzi wa jinsia moja, lakini pamoja na hayo utafiti huo umezua mzozo mkali baina ya walio tayarisha programu hiyo na watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja nchi humo
Hata hivyo watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani wanadai kwamba wame fanikiwa ku-unda programu hiyo ambayo inaweza kuangalia uso wa mtu na maumbile yake na kutofautisha kati ya wapenzi wa jinsia moja na wapenzi wengine.
Katika utafiti huo, wataalamu hao waliunda programu kwa kutumia picha za wanaume 14,000 wazungu kutoka kwenye tovuti ya kutafuta wapenzi. Walitumia picha kati ya moja na tano za kila mtu na kurekodi msimamo wa mtu kimapenzi kama alivyo jitangaza katika tovuti hiyo ya kuchumbiana.
Wataalamu hao wanasema programu waliyoiunda ilionekana kuwa na uwezo wa kuwatofautisha wanaume na wanawake wapenzi wa kawaida na wapenzi wa jinsia moja kwa asilimia kubwa sana
Katika jaribio moja, programu hiyo ilipopatiwa picha mbili ambapo moja ilikuwa ni basha na nyingine ya mwanamume wa kawaida, ilifanikiwa kuwa tofautisha wawili hao kwa asilimia 81 na kwa upande wa wanawake, ilifanikiwa asilimia 71.
Gazeti la Economist ambalo lilikuwa la kwanza kuchapisha utafiti huo limesema miongoni mwa upungufu wa programu hiyo ni kwamba imeangazia zaidi Wazungu na pia imetumia picha kutoka kwa mitandao ya kuchumbiana, ambazo mara nyingi huwa zinaashiria msimamo wa watu.
Mashirika mawili ya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja yametoa taarifa kushutumu utafiti huo na kusema kwamba unaweza kutumiwa kuwadhuru wapenzi wa jinsia moja.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.
Chanzo : BBC Swahili