Hivi karibuni raisi mteule wa marekani Donald Trump alipanga kukutana na viongozi au wawakilishi wa makampuni ya teknolojia ya marekani. Kwa mojibu wa tovuti ya habari za teknolojia ya Tech cruch Donald Trump aliongea na viongozi kutoka kampuni ya Google, Microsoft, Amazon, Apple, Oracle pamoja na Facebook.
Jambo jipya lililo tangazwa na tovuti mbalimbali za teknolojia ambalo huenda lilitokana na mkutano huo, ilikua ni pale raisi huyo mteule atakapo taka kuanzisha jalada maalum la kusajili waislamu wote wanaoishi nchini marekani jalada hilo liliopewa jina la Muslim registry.
Kampuni ya Twiiter ndio iliyokua ya kwanza kusema kuwa haito weza kumsaidia raisi hiyo mteule kutengeneza jalada hilo la Muslim registry, kwa mujibu wa tovuti ya Recode hadi kufikia jana kampuni za Apple, Facebook, Google, IBM pamoja na Uber nazo pia zilisema kuwa hazitoweza kutoa msaada wowote kwa Trump ili kufanikisha kuanzisha jalada hilo.
Katika kauli mbalimbali za viongozi na wawakilishi wa makampuni hayo ya teknolojia kama zilizivyo andikwa na tovuti ya Buzzfeed wawakilishi wengi wa makampuni hayo walisema kuwa, hawaja ambiwa kufanya hivyo lakini ikitokea hivyo basi watakataa moja kwa moja. Kwani kila mtu ana haki ya kutumia huduma za makampuni hayo bila kuangali dini wala rangi.
Hata hivyo kwa mujibu wa video hiyo hapo juu kutoka CNN, Kris Kobac Katibu wa jimbo la kansas nchini marekani ambaye kwa sasa ndio aliyekua anamsaidia trump katika swala zima la wahamiaji alisema kuwa hakuna jambo kama hilo wala hakuna majadilianio ya kuanzisha jalada hilo.