Nchini China, teknolojia kwa upande wa polisi imezidi kuwa kubwa sana na kurahisishia kazi kwa polisi wa nchini humo hasa pale linapokuja swala la kukamata wahalifu haswa wanao ingia na kutoka nchini humo.
Teknolojia hiyo mpya inayo husisha miwani maalum zenye teknolojia ya kutambua uso (facial recognition) zinauwezo wa kutambua baadhi ya wahalifu kupitia kifaa maalum ambacho huangalia sura ya mtuhumiwa na kuwasilisha kwenye datakazi (database) ya wahalifu na mara moja polisi hupewa taarifa kuhusu mtuhumiwa na hatimaye mtuhumiwa huyo kukamatwa.
Kwa mujibu wa tovuti ya People’s Daily ya nchini humo, tayari teknolojia hiyo imewezesha kukamata wahalifu mbalimbali wanao husishwa na makosa makubwa ya uhalifu nchini humo zaidi ya 26 pamoja na wahalifu wengine wanao ingia kwenye nchi hiyo kwa majina pamoja na hati za kusafiria za kugushi.
Kampuni inayohusika na utengenezaji wa miwani hizo, LLVision Technology Co. kupitia msemaji wake imesema kuwa teknolojia hiyo mpya ina uwezo wa kuangalia utambulisho wa watu kutoka kwenye datakazi (database) ya watu zaidi ya 10,000 na kurudisha majibu kwa haraka ndani ya sekunde 0.1 hivyo kufanya miwani hizo kuwa na uharaka zaidi pale inapo hitajika ku-mtambua muhalifu kwa haraka bila kumuangalia sana kwa muda mrefu.
Kampuni hiyo ambayo imebobea kwenye utengeneza wa vifaa vya kutambua uso (facial recognition) imesema teknolojia hiyo kwa sasa bado iko kwenye majaribio na haitapatika kwa wateja wengine kutokana na hofu ya usalama wa usiri inayotokana na teknolojia hiyo.
Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya Teknolojia, Pakua sasa App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia unaweza kujiunga na Channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili kujifunza mambo yote ya Teknolojia kwa njia ya video.