Teknolojia inazidi kukuwa kila siku kiasi kwamba ni ngumu sana kuweza kujua mambo yote kuhusiana na teknolojia. Lakini leo hapa Tanzania Tech tunakuletea aina mpya za teknolojia ambazo huenda hadi leo ulikuwa huzijui, basi bila kupoteza muda lets get to it.
5. Geopress
Geopress ni aina mpya kabisa ya teknolojia ya kutakatisha maji, Geopress ni chupa ya maji ambayo ina uwezo mkubwa wa kutakatisha maji ya kunywa. Kwa kutumia chupa hii unaweza kunywa maji ya sehemu yoyote ile iwe ni kwenye mito, mabwawa ya maji safi au hata maji ya bomba bila hata kufikiria kuchemsha, Geopress inauwezo wa kuondoa vijidudu vyote vya kwenye maji ikiwa pamoja na kutakatisha maji hayo na kuondoa harufu. Chupa hii hufanya kazi yote hii pale unapo funika mfuniko wake ambao ndio hufanya kazi ya kutakatisha maji kwaajili ya kunywa.
4. Solar Roads
Nishati ni kitu cha muhimu sana ndio maana wanzetu hufikiria zaidi linapokuja swala hili. Solar roads ni aina mpya ya barabara za lami ambazo zina tengenezwa kwa kutumia panel maalum za solar kwaajili ya kutengeneza umeme. Kwa kuwa barabara nyingi zinakaa kwenye jua kwa muda mrefu barabara hizo za solar zinaweza kutengeneza umeme wa kutosha kabisa kwa matumizi ya kila siku. Aina hii ya teknolojia haijaishia kwenye barabara tu bali pia unaweza kutengeneza parking yenye solar au hata uwanja wenye solar.
3. Coolest Mouse Ever
Kila mtu anajua ni lazima kutumia Mouse ili kuweza kutumia kwa usahihi kompyuta yako, lakini kadri siku zinavyo kwenda nadhani tutakuwa hatuitaji kabisa mouse. Kutana na pete ambayo inaweza kuwa mouse ya kompyuta yako, kwa kutumia pete hii unaweza kuendesha kompyuta yako kwa haraka na kwa urahisi mahali popote unapokuwa, sidhani kama na aja ya kuelezea sana najua umesha angalia video hapo juu.
2. Dolfi
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hawapendi kufua basi lazima utaipenda hii. Kutana na Dolfi, Dolfi ni aina mpya ya mashine ya kufulia ambayo iko sawa kwa ukubwa na simu yako ya mkononi. Dolfi inaweza kufua nguo kwa dakika 30 na bila kutingisha nguo hiyo kama mashine nyingine za kufua, mashine hii inatumia mionzi maalum ambayo hii hutoa mitetemeko ambayo ndio inaweza kufanya uchafu kutoka kwenye nguo kwa haraka. Dolfi inaweza kufua nguo za aina zote bila kuvujisha au kuchujisha rangi, kifupi ni kwamba unaweza kufua nguo ya aina yoyote kwa kutumia mashine hii.
1. Lumzag
Lumzag ni aina mpya kabisa ya begi janja lenye uwezo wa kufanya mambo ambayo begi la kawaida haliwezi kufanya. Begi hili la Lumzag linakuja na uwezo wa kamera ambayo inaweza kuonyesha nini kinaendelea nyuma yako, pia begi hili linakuja na Anti Theft ambayo inaweza kukupa taarifa pale mtu atakapo taka kuchukua begi lako, pia utakapo kuwa mbali na begi hili huweza kukupa taarifa kupitia simu yako. Begi hili pia lina uwezo wa kukupa taarifa pale unapo sahau kitu ambacho kilikua ndani ya begi hilo, hivyo hakuna kusahau tena. Begi hili linakuja na uwezo wa kuchaji simu, na kompyuta na pia unaweza kuchaji simu yako bila kutumia waya.
Mbali ya yote, begi hili linakuja na Wifi ambayo unaweza kutumia popote pale ulipo hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi wa kuishiwa na bando. Begi hili kwa sasa bado halipo sokoni ila unaweza kutoa oda yako kupitia hapa.
Na hizo ndio aina mpya 5 za teknolojia ambazo inawezekana ulikuwa hujui, Tuambie kwenye maoni hapo chini ni aina pi ya teknolojia ambayo umeipenda zaidi.. Kama una swali au maoni pia unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
Ama kweli tecnolojia inakua kwa kasi kwa makadilio hilo begi litaghalim kiasi gani?