Ukweli ni kwamba teknolojia imekuwa ni msaada mkubwa sana, sio kwa hivi sasa pekee, bali hata siku zinazokuja teknolojia itakuwa msaada mkubwa sana kwa watu wengi watakao itumia. Kuliona hili, leo kupitia makala hii ningependa nikuonyesha baadhi ya teknolojia ambazo huwenda ulikuwa huzijui teknolojia mbazo kwa namna moja ama nyingine zimekuwa msaada kwa jamii.
Nategemea nikushangaze angalau kidogo hivyo jitahidi kusoma angalau asilimia 80 ya makala hii kwani na uhakika ukimaliza lazima utasema “hakika teknolojia imefika mbali sana”. Basi bila kuendelea kupoteza muda wako kwa maneno mengi twende tukangalie teknolojia hizi mpya.
TABLE OF CONTENTS
Camp Stove 2
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wameshawahi kutumia moto wa kuni kwa namna moja ama nyingine basi huenda ukapenda jiko hili la kisasa. Kutana na Camp stove 2, hili ni jiko la kuni ambalo linakupa uwezo wa kuchaji smartphone yako pamoja na kupata nishati ya moto wa kuni bila kupata adha ya moshi. Jiko hili dogo limetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa kiasi kwamba alitumii kuni nyingi lakini linaweza kutoa kiasi cha kutosha cha nishati. Mbali ya yote, jiko hili linakuja na uwezo wa kipekee wa kuweza kuchaji vifaa mbalimbali kutokana na joto linalo tokana na nishati ya moto wa kuni pale unapo tumia kupikia.
Smart Bolt
Kama wewe ni fundi kwa namna moja ama nyingine basi lazima utaipenda smart bolt. Kutana na Smart bolts, hii ni bolt janja ambayo ina uwezo wa kuonyesha kama bolt imekazwa vizuri au lah. Smart Bolt inakuja na sehemu yenye alama katikati ambayo sehemu hiyo hubadilika rangi kila unapozungusha bolt hiyo ili kuonyesha kiwango cha mkazo wa bolt hiyo. Pia unaweza kutumia mwongozo wa karatasi maalum yenye rangi ili kuonyesha kiwango cha mkazo wa bolt hiyo.
Lua
Kutana na Lua, Lua ni chungu cha kidigital cha kupandia maua, chungu hichi sio kama vyungu vingine kwani hichi kina uwezo wa kukujulisha jinsi MMEA UNAVYO JISIKIA. Kwa kutumia kioo chenye sura ya emoji mbele ya chungu hicho, utaweza kujua kama mmea unahitaji maji au mwanga au kama mmea unakauka kwa kukosa virutubisho. Yote hayo huwezeshwa kwa kutuma teknolojia ya kisasa ambayo hupima kiasi cha unyevu kwenye mmea. Chungu hicho pia kina sense maalum ambayo hutambua vitu mbalimbali vinapokuwa karibu yake.
Mashine ya Kupalilia
Kama tunavyojua hakuna kazi ya muhimu shambani kama kupalilia. Kwa kuzingatia hayo, kutana na mashine hii ya kisasa ambayo inayo uwezo mkubwa wa kungoa majani yasiyotakiwa shambani ikiwa pamoja na kupulizia dawa kwenye mimea kwa pamoja. Mashine hii hutumia umeme wa solar na huendeshwa kwa kutumia smartphone. Pale mtumiaji anapowasha mashine hiyo mara moja huiacha na yenyewe huendelea na palizi bila mtu kuendesha mashine hiyo.
Mashine za Kumenya
Kutana na mashine maalum ya kusaidia kumenya matunda ya aina mbalimbali. Mashine hizi zimetengenezwa maalum kumenya matunda ya aina zote ndani ya sekunde chache, mashine ndogo zinamenya matunda madogo kama chungwa na mashine kubwa zinatumika kumenya matunda makubwa kama tikiti, maboga, mananasi na matunda mengine pia zipo mashine nyingine za kumenye ndizi pamoja na viazi. Mashine hizi zimetengenezwa na kampuni inayoitwa pelamatic.
Super Million Hair
Kutana na kifaa hichi chenye uwezo wa kuongeza nywele kwa aliye na nywele chache na nyepesi, pia kina uwezo wa kuziba kipara na kufanya nywele zijae na ziwe nyeusi. Kifaa hichi sio kama ile dawa ya piko, bali hichi kinatoa material kama unga ambao hushikana na nywele zako moja kwa moja na hudumu kwa muda mrefu. Unga huo hauingii maji wala hautoki pale utakapo pigwa na upepo au kunyeshewa na mvua.
Prynt
Kutana na kifaa hichi chenye uwezo wa ku-print picha moja kwa moja kutoka kwenye simu yako. Kifaa hichi kina uwezo wa ku-print picha ndani ya sekunde 30, mbali na hayo kifaa hichi kinakuja na app ambayo inaweza kuweka video kwenye picha ya kawaida ya karatasi. Ili kuangalia video iliyopo kwenye picha ya karatasi unatumia kamera ya simu yako na kupitia kioo cha simu yako moja kwa moja utaona video iliyopo kwenye karatasi.
Rotimatic
utana na mashine ya kupika chapati, mashine hii inauwezo wa kukanda unga na kupika chapati ndani ya muda wa sekunde 90 (dk 2). Unachotakiwa kufanya ni kuweka unga sehemu yake, maji sehemu yake na mafuta kisha washa mashine hiyo na chagua idadi ya chapati unazotaka. Mashine hii inatumia mfumo wa AI kuweza kupika chapati makini.
Najua unaweza kuwa unalalamika kuhusu bando hivyo kwa leo naomba nishie hapo, kama unataka kujua zaidi kuhusu teknolojia mpya unaweza Kusubcribe kwenye channel yetu kupitia mtandao wa YouTube kwani huko huwa tunangalia teknolojia mpya kama hizi kila siku. Kama unataka kujua teknolojia nyingine mpya unaweza kusoma hapa.