Kampuni ya Tecno imetajwa kwenye moja ya makampuni ambayo simu zake zitakuwa za kwanza kupata mfumo mpya wa Android 10 Q. Kupitia mkutano wa Google I/O 2019 kampuni hiyo imetajwa miongoni mwa makampuni mengine kumi na tatu ambayo simu zake zitapata mfumo huo za kwanza.
Hata hivyo, kampuni ya Google imatangaza kuwa tayari simu mpya zaidi ya 10 kutoka kwa makampuni hayo 13 zimetangazwa kupata toleo la majaribio kuanzia siku ya jana. Simu hizo zilizotajwa ni pamoja na
- Asus Zenfone 5z
- Essential Phone
- Huawei Mate 20 Pro
- LG G8 ThinQ
- Nokia 8.1
- OnePlus 6T
- Oppo Reno
- Realme 3 Pro
- Sony Xperia XZ3
- Tecno Spark 3 Pro
- vivo X27
- vivo NEX S
- vivo NEX A
- Xiaomi Mi 9
- Xiaomi Mi Mix 3 5G
Kwa sasa kama wewe ni mmoja wa watu wenye simu moja kati ya hizo hapo juu basi unaweza kujaribu moja kwa moja mfumo mpya wa Android 10 Q ambao kwa sasa uko kwenye majaribio ya awamu ya tatu (Android Q beta 3). Ili kujaribu tembelea ukurasa HUU HAPA na simu yako kisha bofya sehemu ya View your eligible devices.
Hii ni mara ya kwanza kwa simu ya TECNO kuweza kutajwa na Google kama washirika kwenye kujaribu mfumo mpya wa Android, hatua hii ni nzuri sana kwa kampuni ya TECNO kwani inaonyeshakuwa kampuni hiyo kwa sasa imekuwa na inaendelea kutambulika kwenye nchi mbalimbali tofauti na Afrika.
Kwa sasa kama unataka kujua zaidi kuhusu simu mpya za Tecno spark 3 na Spark 3 Pro, unaweza kusoma hapa kujua sifa kamili pamoja na bei zake hapa nchini Tanzania.