Kampuni ya simu za mkononi TECNO imezindua duka kubwa la simu, maarufu Smarthub jijini Arusha ambalo linatoa huduma mbalimbali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo mwishoni mwa wiki, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw. Benjamin Maneno ambaye pia alikuwa ndiye mgeni rasmi, alisema.
“Kwa karne tuliyofikia hivi sasa, matumizi ya smartphone hayaepukiki, kwahiyo tunachoomba sasa wananchi waje kwenye maduka ya TECNO kwaajili ya kupata fursa ya kupata vipato kupitia simu za TECNO, sio kutumia kuchati tu lakini unapotumia intaneti kwenye simu za TECNO unaweza kufanya biashara na hata kupata masomo”
Bw. Benjamin Maneno Mwakilishi wa Mkurugenzi Jiji la Arusha akipiga makofi mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa dukala kisasa la TECNO.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha akiweka sahihi yake katika bango maalum lililokuwa limeandaliwa na TECNO
Kwa upande wake Msimamizi wa Mauzo kanda ya Kaskazini Bw. Kassim Haji alisema, “Tunawakaribisha wateja wa mikoa ya karibu katika Duka hili jipya la TECNO “Smarthub”, Kuna faida nyingi ambazo wateja watanufaika nazo ikiwemo huduma ya kupata fursa ya kununua bidhaa zetu za simu kwa bei nafuu, vifaa vya simu, kupewa elimu ya bure kuhusiana na matumizi, sifa na mifumo ya simu, vilevile kwa mteja atakayenunua simu katika msimu huu wa Valentine, ataingia kwenye droo ya kujishindia friji kubwa”
Msimamizi wa Mauzo kanda ya Kaskazini Bw. Kassim Haji akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya dukio la uzinduzi wa duka la TECNO.
Uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali wa TECNO uliambatana na burudani huku baadahi ya wadau wakipendekeza mambo mbalimbali yanayohusu kupotea kwa simu.
“Leo tunawashukuru sana uongozi mzima wa TECNO kwa kujali mahitaji ya wananchi wa jiji la Arusha kuamua kufungua duka jipya la kisasa. Uongozi mzima wa TECNO wajaribu kuwafundisha wananchi wanapokuja kununua simu mambo ya msingi wanayoweza kuhifadhi ili baadaye simu ikipotea waweze kui-track” Alisema mdau Bw. Severine Kinabo.
Mhudumu wa Duka Jipya la TECNO akiwaelekeza mifumo ya simu za TECNO.
TECNO imedhamiria kupanua wigo wa huduma zake na kuzisogeza karibu na wateja wake kwa kufungua maduka makubwa ya kisasa yenye huduma zote ambapo wateja hawatatumia muda mrefu kupata huduma hizo.
Hata hivyo TECNO tayari imeshaweka maduka makubwa katika majiji yote makubwa Tanzania ikiwemo, Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya.