Kampuni Mama ya TECNO Kuja na Huduma ya Pesa ya PalmPay

Huduma mpya ya kutuma na kupokea pesa kutoka TECNO
Tecno Palmpay Tecno Palmpay

Wakati kukiwa na ongezeko kubwa la huduma za kifedha kupitia simu za mkononi, sio kitu cha kushangaza sana kuona kampuni kubwa zenye uwezo wa kifedha kufikiria kuingia kwenye biashara hiyo ambayo inaonekana kuwa na faida kubwa hapa barani Afrika.

Kwa mujibu wa tovuti ya allafrica, Vodacom Tanzania ilipata ongezeko la faida hadi kufikia bilioni 47.6bn mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka 2017, huku asilimia kubwa ya faida hiyo ikitajwa kusababishwa na huduma za M-Pesa zinazotolewa hapa nchini Tanzania. Mbali na hayo kuonyesha kuwa biashara hiyo ya kifedha kupitia simu za mkononi inakuwa kwa kasi, hivi karibuni tumesikia ujio wa huduma za kifedha kama Branch, Tala na nyingine kama hizo ambazo zinategemewa na watanzania wengi kwaajili ya kupata mikopo ya haraka kupitia simu za mkononi.

Advertisement

Pengine kukuwa kwa teknolojia pamoja na biashara ya simu kuendelea kuwa nzuri kwa kampuni kama TECNO, ndio sababu kampuni mama ya TECNO Mobile inayoitwa Transsion imeamua kufikiria kuja na huduma mpya ya kifedha kupitia simu ya mkononi inayoitwa PalmPay.

Kwa mujibu wa tovuti ya Techweez, kampuni hiyo ya Transsion imeingia makubaliano na kampuni ya NetEase ili kuleta huduma hiyo hapa Afrika ambayo imesajiliwa chini ya jina la kampuni ya Transsnet Payment Limited. Hata hivyo techweez imeandika kuwa huduma hiyo mpya ya Palmpay itakuwa inatoa huduma za kutuma na kupokea pesa, kuomba mikopo pamoja na huduma za kulipia bili pamoja na kununua muda wa maongezi.

Mbali na hayo, kwenye huduma hiyo mpya ya PalmPay kutakuwa na sehemu inayoitwa PalmPoints sehemu itakayo kuwa inakupa pointi kutokana na huduma unazotumia, pointi ambazo baadae unaweza kuzibadili na kupata mapunguzo ya bei, ofa mbalimbali au muda wa maongezi.

Hata hivyo kwa mujibu wa techweez, kampuni hiyo mama ya TECNO Transsion inaweza kusukuma zaidi huduma yake hiyo kwa kupitia njia ya kuweka programu au app ya huduma hiyo kwenye kila simu za tecno zitakazokuwa zinaingia sokoni. Kwa mujibu wa ripoti hiyo huduma hiyo inatarajiwa kuja kwanza kwa nchi ya Kenya, Tanzania na Nigeria kabla ya kufikia nchi nyingine hapa barani Afrika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use