Kuelekea mwisho wa mwaka 2021 kampuni ya simu za mkononi TECNO yenye mashabiki wengi hasa upande wa simu janja inatarajiwa kuzindua toleo jipya la mfululizo wa simu zake aina ya TECNO Camon 18 yenye ubora ulioboreshwa hasa upande wa picha na video.
Series ya CAMON imekuwa ikiaminika kuwa na simu zenye kamera kali kutoka kwenye kampuni hiyo, japo simu hiyo haijatambulishwa rasmi lakini tayari kuna tetesi huenda simu hiyo ni TECNO Camon 18.
TECNO Camon 18 inasemekana kuja kuwa suluhisho kwa wenye uhitaji mkubwa wa kamera katika kazi za kila siku hata kwa waandishi wa habari itawasaidia katika kuchukua matukio kadha wa kadha ambapo ina Mega Pixel 64.
Simu hii inayosemekana kuwa camon 18 ndiyo simu ya kwanza TECNO kuwa na GIMBAL CAMERA hii ni kamera ya hali ya juu sana katika mfumo mzima wa uchukuaji video kuwahi kutokea TECNO ambapo inaweza kurekodi video HD katika mazingira yoyote yale hata kama mchukuaji video anakimbia au kutembea lakini video haitotingishika.
Mfumo wa ufanyaji kazi wa Gimbal camera
Pia simu hii ya CAMON 18 ina kamera yenye uwezo mkubwa wa ku-zoom mara 60X Zaidi na kufanya kitu kilichokuwa mbali na kuwa karibu Zaidi. Bila kusahau main kamera ya CAMON 18 ina mega pixels zipatazo 64 za kukuwezesha kupiga picha safi katika mazingira ya usiku na mchana.
Mfumo wa camera unavyozoom mara 60x zaidi
Pia wameboresha uwezo wa kuhifadhia kumbukumbu ni mkubwa zaidi ambapo itakuwa na 256GB ROM kwa 8GB RAM hivyo kuzidi kumvutia mteja kumiliki simu hii yenye uwezo mkubwa zaidi. Kufahamu Zaidi kuhusiana na CAMON 18 tembelea: shorturl.at/isvzM