Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya TECNO yazindua Simu Mpya za Camon 16

Hatimaye kampuni ya TECNO imezindua simu mpya za Camon 16 zenye kamera kubwa
Kampuni ya TECNO yazindua Simu Mpya za Camon 16 Kampuni ya TECNO yazindua Simu Mpya za Camon 16

Mara baada ya tetesi za ujio wa toleo jipya la simu za Camon 15, hatimaye hapo jana kampuni ya TECNO imezindua simu zake hizo mpya zikiwa kwa matoleo matatu ya TECNO Camon 16, Camon Pro na Camon 16 Premier.

Hadi sasa tayari simu ya TECNO Camon 16 Premier ndio inayopatikana sokoni, huku simu za Camon 16 na Camon 16 Pro zikiwa bado hazipatikani kwa sasa.

Advertisement

Kwa upande wa sifa, hadi muda ambao tuna andika makala hii, sifa za TECNO Camon 16 Premier ndio zinazo julikana huku sifa za simu nyingine zikiwa bado hazijajulikana.

Sifa za TECNO Camon 16 Premier

TECNO Camon 16 Premier inakuja na kioo cha inch 6.9 huku kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, kwa juu ya kioo hicho kuna kamera mbili za Selfie kamera moja inakuja na uwezo wa Megapixel 48 na nyingine ikiwa na uwezo wa Megapixel 8. Kamera zote za mbele zina uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps.

Kampuni ya TECNO yazindua Simu Mpya za Camon 16

Kwa upande wa nyuma, Camon 16 Premier inakuja na kamera nne huku kamera kuu ikiwa na Megapixel 64 na nyingine ikiwa na Megapixel 8 huku nyingine mbili zikiwa na Megapixel 2 kila moja. Kamera hizo zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K.

Kwa upande wa sifa za ndani, Camon 16 Premier inaendeshwa na processor ya MediaTek Helio G90T, yenye uwezo wa CPU ya hadi Octa-Core 2x 2.05GHz Cortex-A76 & 6x 2.0GHz Cortex-A55. Kwa upande wa RAM simu hii inakuja na RAM ya GB 8 pamoja na uhifadhi wa ndani au ROM ya GB 128, pia unaweza kuongeza uhifadhi huu kwa kutumia memory card ya hadi GB 256.

TECNO Camon 16 Premier inatumia mfumo wa uendeshaji wa Android 10, mfumo ambao juu yake kunao mfumo mpya wa TECNO HiOS 7.0 mfumo huo unakuja na sehemu mpya mbalimbali ikiwa pamoja na sehemu mpya ya Dark Mode na mambo mengine mbalimbali.

Kampuni ya TECNO yazindua Simu Mpya za Camon 16 Kampuni ya TECNO yazindua Simu Mpya za Camon 16

Battery ya Camon 16 Premier inakuja na uwezo wa 4500 mAh battery huku ikiwa na teknolojia ya Fast Charging yenye uwezo wa hadi 33W (SuperCharge), Kwa sifa zaidi soma hapa.

Mbali na simu hizo, TECNO pia imezindua smart watch maalum kwa simu hiyo, pamoja na wireless headphones. Habari zaidi kuhusu vifaa hivi tutawaletea hapo baadae.

Kampuni ya TECNO yazindua Simu Mpya za Camon 16

Bei ya TECNO Camon 16 Premier

Kwa upande wa bei, Camon 16 Premier inategemewa kuanza kupatikana kwenye nchi mbalimbali hapa Afrika ikiwemo Kenya, kwa bei ya makadirio kuanzia TZS 580,000. Kumbuka bei hii ni ya makadirio na inaweza kubadilika pale simu hii itakapo tangazwa rasmi hapa Tanzania.

Kujua sifa pamoja na bei ya TECNO Camon 16 na Camon 16 Pro, hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech, au unaweza kuangalia kupitia tovuti yetu ya priceintanzania.com.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use