Kampuni kinara ya simu za mkononi TECNO ndio kampuni inayosemekana na wadadisi wa masuala ya teknolojia ya simu kuwa huenda ndio itakayoleta teknolojia ya kamera ya simu ambayo kwa mara ya kwanza katika tasnia ya masuala ya simu janja Tanzania itakata kiu kwa watumiaji wa simu hizo hasa kwa upande wa kamera, betri na muundo wa simu yenyewe.
Toleo la simu hiyo halijawekwa wazi bado lakini imebainishwa kuwa litatoka kwenye mfululizo wa matoleo ya TECNO CAMON na litaachiwa sokoni ndani ya mwezi huu Aprili. Simu hiyo imebainishwa itakuwa na kamera tatu nyuma lensi na flash ambapo kamera kuu ina MP 64.
Teknolojia ya kamera ya simu hii inaelezwa kuwa na uwezo wa kupiga picha mahali popote hata gizani kutokana na kuwa na flash nne zenye uwezo na nguvu kubwa ya kusawazisha picha ing’are sehemu zenye ukungu na giza huku lensi yake ikimwezesha mtumiaji kupiga picha kitaalam zaidi hata kama hana ujuzi wa kupiga picha.
Kwa taarifa zilizotufikia ni kwamba upande wa kamera ya mbele ina MP 32 huku ikiwa tofauti kabisa na simu nyingine kwa namna ilivyoundwa kwani iko ndani ya simu ambapo mtumiaji akitaka kupiga selfie, kamera hii huchomoza kwa juu wengine huita Pop- Up Camera.
TECNO ambayo simu yake ya mwisho katika mfululizo wa CAMON ni CAMON 12, ndio kampuni inayotarajiwa kuleta madiliko haya makubwa ya teknolojia ya kamera za simu kwa mwako huu 2020.
Kwa upande wa sifa nyingine endelea kufuatilia taarifa zetu tutawapa mrejesho mara tu baada ya kupata taarifa rasmi kutoka TECNO.