Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mambo ya Muhimu Kujua Kuhusu Tecno Camon 11 na 11 Pro

Mambo mazuri kwenye simu mpya za Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro
Kizuri kuhusu Tecno Camon 11 na Camon 11 pro Kizuri kuhusu Tecno Camon 11 na Camon 11 pro

Kampuni ya Tecno hivi karibuni imezindua simu mpya za Tecno Camon 11 na Tecno Camon 11 Pro, simu hizi zinakuja na muundo mpya kabisa huku zikiwa na sifa nzuri zaidi. Lakini pamoja na yote ni kweli kuwa kila kizuri hakikosi kasori na yapo mambo mengi sana ambayo kwa upande wangu naona ni kasoro kwenye simu hizi mpya, lakini pamoja na hayo leo tuko hapa kuongelea mambo mazuri ambayo pengine utegemee kuyaona pale unapokuwa na simu hizi mpya za Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro.

Battery

Kwa kuanza labda nianzie upande wa battery, najua kuwa hakuna asie penda simu inayodumu na chaji kwa muda mrefu na kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda simu ya kuchaji mara moja kwa siku basi pengine ni vyema kuangalia simu za Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro.

Advertisement

Kwa mwaka huu kampuni ya Tecno imejitahidi sana kuweka battery kubwa kwenye simu zake hizi mpya kwani simu za Camon 11 na 11 Pro zote zinakuja na battery kubwa ya Li Po yenye uwezo wa 3,750 mAh. Kwa kawaida battery yenye 3,500 mAh inaweza kukutosha kutumia siku nzima lakini nadhani pengine inategemeana na matumizi yako ya kila siku.

Kwa mimi kuanzia nishike simu hii, inaweza kudumu na chaji kuanzia masaa 20 hadi 23 kama natumia sana simu hiyo. Kifupi kwa matumizi yangu ya kila siku naweza kusema Camon 11 na 11 Pro zinaweza kukupa uwezo wa kutumia simu hiyo siku nzima kama ukichaji simu hiyo ikajaa vizuri.

Memory

Upande mwingine ambao ni bora kwenye simu hii ni pamoja na uwezo wa RAM. Ni kweli tumesha zoea simu nyingi za Tecno zinakuja na uwezo mdogo sana wa RAM na mara nyingi hii hufanya simu hizi kushindwa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

Kwa simu hizi mpya za Tecno Camon 11 ni tofauti kidogo kwani kampuni ya Tecno imejitahidi kuweka RAM ya GB 3 kwenye toleo la Camon 11 na mara mbili ya hapo kwenye toleo la Camon 11 Pro. 

Kwa muda wote niliopata kuweza kujaribu simu hii nimegundua inauwezo mzuri sana wa kufungua programu nyingi kwa pamoja, mimi huwa natumia simu sana kwenye kufanya utafiti wa makala mbalimbali hivyo mara nyingi najikuta nimefungua kurasa nyingi sana kwenye kivinjari cha simu yangu na ukweli kwa muda niliotumia Camon 11 nimegundua kuwa inauwezo mzuri wa kufanya hivyo bila wasiwasi.

Kamera

Kwa upande wa kamera Tecno wamejitahidi sana kwe toleo hili la Camon 11 na 11 Pro, Kwa upande wangu mimi binafsi nimependa kamera za nyuma za Camon 11 Pro kuliko Camon 11. Camon 11 Pro iko vizuri zaidi kwani yenyewe inakuja na kamera mbili za nyuma za Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 5 kwa mbele simu hii inakuja na kamera ya Megapixel 24.

Camon 11 yenyewe inakuja na kamera za Megapixel 13 na Megapixel 2 kwa nyuma, huku kwa mbele simu hii ikija na kamera ya Selfie ya Megapixel 16. Kingine kizuri kuhusu simu hizi mbili kwa upande wa kamera ni ujio wa AI kwenye kamera hizi, Kupitia simu hizi mpya utaweza kuchagua aina mbalimbali za picha ambazo kweli zitabadilisha muonekano wa picha zako.

Muonekano

Kitu cha mwisho kwangu ambacho nahisi nimekipenda kwenye simu hii ni muonekano wa simu hii, Tecno Camon 11 na 11 Pro zinakuja na muonekano flani hivi Amazing.. muonekano ambao unafanya ujisikie vizuri ukiwa umeshika simu hiyo hasa kwa wale wapenzi wa simu hizi za Tecno. Kama ulisha wahi kushika Tecno Phantom na ukajisikia vizuri basi ni wazi kuwa simu hii pia ukishika lazima utajisikia vizuri.

Kingine ambacho ni kizuri kuhusu muonekano wa simu hii ni kwenye ukingo wa juu, ukweli mimi sipendi sana simu zenye ukingo wa juu lakin nashkuru Tecno wameweka sehemu ambayo unaweza kutumia kuficha ukingo huo.

Kwa upande wangu hayo ndio mambo ambayo nimependa kwenye simu hizi mpya za Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro. Yapo mambo mengi sana ambayo sijapenda kwenye simu hii kama vile uwezo wa kioo, kamera za mbele, bei za simu hizi ni ghali sana na mambo mengine mengi, lakini kwa sababu nilisha sema hapa tunaangalia mambo mazuri pekee pengine hii kazi nikuachie wewe uniambie kupitia sehemu ya moani hapo chini, Ni kitu gani unahisi hutakipenda kwenye simu hizi za Tecno Camon 11 na Camon 11 Pro..?

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use